BINADAMU HATUPO SAWA

 

BINADAMU HATUPO SAWA

Sura hii inaeleza kinaga ubaga kwamba binadamu hatupo sawa hapa duniani maana yake binadamu hapa duniani ni  kama vidule ambavyo havililingani ambapo katika  vidole kila kidole ni tofauti na kidole kingine,  kuna kidole  kikubwa,kidogo, kidogo zaidi na hivyo  kwa hali hivyo inaeleza kuwa hata binadamu wa Duniani hatupo sawa kabisa.

Hatupo sawa kwa sababu kuna watu wenye maisha ya chini sana na watu wenye maisha ya juu sana. Hatupo sawa kwani pia kuna watu wazima na wenye afya zao na kuna watu wasio wazima ambao hawana afya hata kidogo. Kuna binadamu wenye viungo vyote na kuna binadamu hawana viungo vyote. Itoshe tu kusema kwamba duniani hatupo sawa kabisa kwani hata wewe msomaji wa kitabu hiki haupo sawa na msomaji mwingine wa kitabu hiki.

Binadamu tumetofautiana kwa kila hali kiuchumi, kisiasa, kijamii hata  katika maladhi, chakula, mavazi, hali hii inapelekea  maisha ya dunia kuwa tofauti baina ya mtu moja na mtu mwingine. Zipo familia ambazo haziwahi kunywa hata chain a wala hawajawahi kupika hata chele kilo moja, na zipo familia ambazo watoto wamezoeshwa kula wali kila iitwayo siku.

Kuna baadhi ya binadamu ambao hawafurahii kabisa maisha ya duniani na baadhi wantamani hadi kufa maana wao hulalamika kuwa wao ni kama wasindikizaji wa watu wanaofurahia maisha ya duniani. Huu ni ukweli usiopingika. Mimi mwandishi wa kitabu hiki nimewahi kumuhoji mzee mmoja ambaye aliniambia kuwa amesomeshawatoto wake wote na wtoto wake hao hawamjali yeye kwa lolote na anapata shida kana kwamba hakuwa kusomesha. Wapo baadhi ya binadamu  ambao hawafurahii kabisa maisha ya hapa duniani na wapo wenye fedha nyingi mno ambao hata pa kupeleka fedha hakuna. Akisikia mtu ana shida ya fedha anaanza kushangaa, maana duniani hatupo sawa.

 

Binadamu wa hapa duniani tumetofautiana katika kila hali na hali hii ndio inaweza kuleta majivuno na  unyanyasaji wa kidunia

Mtu mwenye ufahali wa kidunia anaona wenzake hawafai, si lolote na hawana haki yoyote, lakini  upande wa pili wa shilingi (Maana shilingi ina pande mbili)  tofauti zote izi zinakuja kuondolewa na Mwenyezi Mungu ndio maana Mwenyezi Mungu amenituma nitunge kitabu hiki kinachoitwa. KWA MUNGU WOTE NI SAWA. Kwa Mungu     hakuna tofauti katika malazi, mavazi, chakula bali binadamu machoni kwa Mungu ni sawa.lakini kwa maisha ya kifahali, kwa nyumba za kifahari sana.

Mfano halisi tunayo, nchi za ulaya, marekani uarabuni kuna maghorofa ambayo ni marefu sana mengine yanakaribia hadi kufika mbinguni na yanamilikiwa na matajiri wakubwa wa duniani. Magorofa hayo yanaitwa  SKY CREEPER magorofa haya yamejengwa juu sana  lakini kwa Mungu binadamu wote ni sawa inamaana hata Yule anayetokea kwenye nyumba za nyasi kwa Mungu yupo sawa na hawa wanaotokea kwenye maghorofa yaliyopaa angani.  

 

Hivyo binadamu upande wa Mungu tupo sawa wala hakuna cheo maalumu, wala Viongozi kutengewa viti vya peke yao kama ilivyo duniani

 

 

 

 

 

 

 

Maoni

Machapisho Maarufu