DUNIANI KUNA VYEO NA WADHIFA MBALI MBALI
DUNIANI KUNA VYEO NA WADHIFA MBALIMBALI
Ni ukweli usiopingika kuwa duniani kuna vyeo
vya kila aina na vyeo hivyo vimetofautiana kulingana na vyeo na wadhifa wa mtu.
Upande wa vyeo kuna vyeo vya chini na vyeo
vya juu na vyeo hivi vinampa mwanadamu heshima kubwa sana hapa duniani hata anapokuwa anapita kutoka sehemu moja kwenda
sehemu nyingine au anapofanya majukumu
yake binafasi vyeo hivyo vinampa heshima
kubwa sana na hali hii ndiyo inayo mtofautisha binadamu huyo na binadamu
wengine.
Suala la vyeo ni jambo ambalo linajulikana
dunia na vyeo hivyo vimetofautiana kuna vyeo vya juu kabisa vya heshima na vyeo
vya chini. Mfano mimi binafsi ni wakili. Wakili pia anaheshimika sana. Lakini baada ya kifo cheo
nilichonacho siendi nacho mbinguni bali nitaenda na nafsi yangu mimi na sio wakili.
Hata wewe msomaji wangu wa kitabu hiki cheo ulichonacho ni cha hapahapa duniani ukienda mbinguni hakuna tena cheo
wala wadhifa wowote ule wala hakuna saluti tena wala hakuna cha kusema simameni
mheshimiwa anapita.
Mbinguni hakuna kupigiwa makofi wala kutengewa kiti maalumu
mbali mbinguni binadamu wote ni sawa. Wadhifa
wa mtu unabaki duniani baada tu ya mtu kufa na kuzikwa. Mbinguni mtu mwenye
wadhifa roho yake tu ndio inayokwenda ama mbinguni au motoni kutokana na
matendo aliyoyaishi.
Itoshe kusema kinagaubaga kuwa vyeo
tulivyonavyo duniani ambavyo ni vyeo vya kifahari na heshima sana ambavyo vinapatikana
kutokana na kusoma, kuteuliwa au kupewa pasipo kusoma kwa upande wa pili wa shilingi, Kwa Mwenyezi Mungu hakuna cheo chochote kile
ambacho ukifariki unaenda nacho mbinguni.
Vyeo hivi
vya duniani vinabakia hapa hapa duniani kwa hiyo tuzidi kufahamu kwamba
kitabu hiki kinakufundisha mwisho wa
yote na mwisho wa vyeo vyote ni hapa hapa duniani sababu mbinguni wote ni sawa.
MASKINI
NA MATAJIRI TUTUTBU DHAMBI ZETU ILI
WOTE TUMUONE MUNGU
Tunachojifunza kutokana na kitabu hiki cha
Wakili JAMES LUBUS kinaeleza kwamba kwa Mungu wote ni sawa na kwa Mungu hakuna tofauti kati ya masikini na tajiri wala
cheo au wadhifa wowote ule. Bali tajiri na Masikini wote ni sawa machoni pa Mwenyezi Mungu .
Pia kitabu hiki kinawapa faraja sana watu wanaoishi maisha ya chini pamoja
na wazee na wagonjwa kwani maisha ya duniani ni ya kupita tu lakini mwisho wa
yote baada ya kufa Mungu atakupa taji lako unalostahili japo huenda ulionekana mbele
ya walimwengu kama takataka machoni pa watu na haufai kabisa., au mgonjwa
uliyeonekana takataka kutokana na ugonjwa ulionao na mtu ambaye hana viungo vya
Mwili vyote ambaye anadhalauliwa na watu na kuonekana haufai kisa yeye ni
kilema lakini kwa mwenyezi Mungu unathamani.
Kwa hiyo kwa wewe ambaye umetengwa na dunia
hii kutokana na umaskini wako, ugonjwa wako uzee wako au vyovyote vile tambua
kwamba kwa Mungu upo sawa kabisa na wala huna tofauti kabisa na watajiri wa duniani.
Hivyo mwandishi wa kitabu hiki anakupa
faraja kuwa ujione wewe unathamani kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu na unastahili
kupewa haki yoyote kama anazopewa binadamu ambaye hana mapungufu yoyote ya
viungo.
Pia Hata kwa wewe Mzee kumbuka kwa Mungu
wote ni sawa kwa hiyo kitabu hiki ni kizuri sana na kinafaa kusomwa na watu
mbalimbali
Sasa nikuombe jambo moja tu ambalo Mungu
atakusikiliza, nenda kwa padre kaungame dhambi zako zote na Mungu atakusamehe.
Ukiungama dhambi zako zote baada ya kifo chako Mungu atakupokea vizuri sana na
utasherekea vyema mbinguni.
Sasa usipoungama dhambi zako unakuwa umeishi
maisha gani? Yani duniani uteseke na utengwe kulingana na umaskini wako alafu
ukifa tena uende kwa shetani huko ukakutane na Moto wa milele.
TUKISEMA HATUNA DHAMBI
TUNAJIDANGANYA”. Ni baada ya kusoma
Biblia vizuri sana kinagaubaga na kugundua kwamba kuna mistari katika Biblia
inayoeleza bayana kwamba wanadamu tumejawa na dhambi, na kwamba tukisema hatuna
dhambi tunajidanganya wenyewe, na kwamba binadamu tumezaliwa tukiwa na dhambi
ya asili isipokuwa tu, Mama Bikira Maria mkingiwa dhambi ya asili. Madhumuni ya
kuwatungia watu mbali mbali kitabu hiki ni kuendelea kuelimisha wasomaji wa kitabu
hiki kwamba sisi binadamu ni wadhambi, na hivyo ili tuweze kupata uzima wa
milele, inabidi dhambi zetu tuweze kutubu. Kwa hiyo, kitabu hiki ni meli ya
kukuvusha juu ya maji ili usizame bali ukamuone Mungu. Kwa tafsiri nyepsi
kitabu hiki kinakusaidia wewe kumuona Mungu kwa kutubu dhambi zako. Hapo
inakuwa ni kama tiketi ya moja kwa moja kutoka duniani kwenda Mbinguni.
Pia kitabu hiki kimeeleza
kinagaubaga kuwa moja ya Sakramenti za
Wakatoliki ni sakramenti ya kupata Komunio. Tunampokea Yesu kupitia umbo la
mkate na divai. Hiyo ni Imani kali ya
kanisa katoliki . Yesu Kristo anakuwa yuko ndani ya moyo wako. Na Yesu Kristo
ili aweze kuwa ndani ya moyo wako inatakiwa moyo wako wewe uwe na moyo ambao ni
moyo msafi. Yesu Kristo hapendi nyumba ambayo siyo safi, nyumba ambayo ina
wageni wengi na hapo ni pale unapo karibisha vitu vingi ndani ya moyo wako, kunakuwa
na chembechembe za wizi ndani ya moyo wako.
Chembe
chembe za ushirikina, na chembe za uchawi ndani ya moyo wako. Ndani ya
moyo wako kunakuwa na kiburi na dharau ya kutokumtii, mke au mume ndani ya moyo
wako unakuwa na wapangaji wengi. Yesu anataka nyumba iwe haina mpangaji yoyote
yule. Hivyo mwandishi wa kitabu hiki anakushauri wewe msomaji wa kitabu uondoe
wapangaji wote na baki Yesu peke yake.
Njia pekee ni kufukuza wapangaji kupitia kutubu dhambi zako na unatakiwa
kuungama kwa padre
BARIKIWA SANA
30.12.2025

Maoni
Chapisha Maoni
thank you very much asante sana