FAIDA YA KUMSIFU MUNGU

 

SURA YA TANO

 FAIDA YA KUMSIFU MUNGU.

Faida za kumsifu Mungu ni Nyingi sana kuliko hata hasara ya kutokumsifu Mungu. Tayari unapokuwa unakuwa umeungana na waumini wengine katika kumsifu Mungu unakuwa tayari  umeanza kuonja utakatifu wa Mungu kwa kuungana na malaika na watakatifu wote ambao wako mbinguni. Ambao na wenyewe wanamsifu na kumtukuza Mungu . Kupitia kumsifu Mungu inakupa na wewe haki ya  kumpenda Mungu na kumsifu Mungu. Inakupa haki ya kuonja sifa za Mungu. Inakupa haki ya kuungana na malaika na watakatifu huko mbinguni. Maandalizi ya kujiandaa kwenda kumsifu na kumwona Mungu kwa macho yako mwenyewe (LIVE)

Faida za kumsifu Mungu ni kubwa sana. Maana yake HAKUJAWAHI kuwa  na furaha nzuri sana duniani kama ile ya kuungana na Mungu katika  kumsifu Mungu. Hivyo ukimsifu Mungu kwelikweli utapata faida zifuatazo

Mungu atasikiliza maombi yako yote ya nyuma na utaona  mabadiliko ya tofauti ya hali ya zamani na hali ya sasa. Mungu atakuponya na magonjwa mbalimbali hata kama umeteseka kweli kweli na magonjwa hayo. Mungu atakuepusha  na ajali mbalimbali. Mitego ya maadui  ambayo maadui  wamekutega haiwezi kukushika hata siku moja badala yake mitego hiyo itawanasa ndugu  zao. Malaika na watakatifu ambao mtunzi wa kitabu hiki anaungana nao kupitia sifa Mungu atawatuma wakulinde  vyema siku zote. Na hivyo utakuwa unakanyaga nyayo ambazo Mungu amekanyaga hivyo hakuna wa kukuzuru. Utakuwa unakanyaga mguu ambao amepita Mwenyezi Mungu  na hivyo unakuwa unakanyaga sehemu salama kabisa. Hata Gari ambalo  wewe unaendesha au ambalo umelipanda , matairi yale yanakanyaga kwenye miguu ya Mungu, yani unapita barabara ambayo Mungu ameshapita.   Faida ya kumsifu Mungu ni kubwa sana kuliko kutokumsifu  kabisa.  Mfano haii kupitia kitabu hiki ambacho utasoma bure kwenye mtandao, mtunzi wa kitabu hiki pamoja na kwamba ana cheo kikubwa sana, Wakili Msomi ameweka uwakili wake pembeni na ameamua kujishusha na kuwa kama mkulima wa kawaida tu kwa ajili ya kumsifu Mungu. Hivyo faida za kumsifu Mungu ni kubwa sana kwani zinakuwezesha hata wewe msomaji kupata kile unachostahili kwa Mwenyezi Mungu. Na hivyo nasisitiza ukiwa na nafasi nzuri ya kumsifu Mungu kwa nafasi yako, msifu Mungu kadri atakavyoona inafaa. Msifu Mungu kadiri atakavyo  kuongoza. Maana maisha ya duniani ni mafupi sana ipo siku utahitaji kumsifu Mungu utakuwa umechelewa kabisa.  Na haya yote ili yafaanyike muombe Mungu akupe Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu huyohuyo ndiye ambaye anaweza kukuongoza kama alivyo muongoza mtunzi wa kitabu hiki  kukitunga hadi wewe kukisoma na vyote hivi amevitoa kichwani na wewe msomaji amini ninachokuambia . Siwezi kusema uongo nitende dhambi ya bure kwa kukudanganya  mimi nakueleza ukweli kuwa sijanakili sehemu yoyote ile katika internet. Mwongozo huu umetokana na kipaji cha Roho mtakatifu cha kutunga vitabu. Wapo wanaosema kuwa natunga vitabu vifupi sana. Mungu alivyokupa ndio hicho kisome. Kitabu kikiwa kikuwa sana watu wanaona uvivu kusoma . Kipaji ambacho mtunzi wa kitabu anacho Wengi walitamani wawe kama mimi, mtunzi wa kitabu. Lakini mimi ni nani mbele ya Mwenyezi Mungu? Mungu amenipa kipaji hiki ambacho ni kipaji adimu sana. Hivyo basi, faida ya kumsifu Mungu ni kubwa sana na hivyo unapata baraka. Kutoka kwake Mungu mwenyewe. Tayari umepata neema kwake Mwenyezi Mungu ambaye ndiye pekee anayestahili kupata sifa ukimsifu Mungu pia.

Ukiwa duniani unapata (confidence) kujiamini kwamba una kinga ya Mungu na hiyo kinga itakukinga dhidi ya wachawi hawataweza kukugusa kabisa kamwe kama una msifu Mungu.  Unaacha alama za Mungu kinywani mwako na hivyo kumfanya Mungu kuwepo na wewe na kuishi na wewe. Hivyo msomaji wa kitabu hiki binafsi nakushauri uwe unamsifu Mungu kwa kuungana na malaika na watakatifu ambao wapo mbinguni kwa ajili ya sifa na utukufu wa Mwenyezi Mungu. Mungu akubariki sana. Barikiwa sana. Mungu akubariki sana.

 

LEO CHRISMASS TAREHE 25.12.2025

Maoni

Machapisho Maarufu