KITABU CHA KWA MUNGU WOTE TUPO SAWA

 

Kilichonichemsha mpaka nikatunga kitabu hiki cha Kwa Mungu wote ni saw ni kutoa elimu mbalimbali baada ya kuona dunia hii hatupo sawa. Dunia hii haiku sawa kwa sababu kuna matabaka baina ya Masikini na Matajiri, Mwenye uwezo na wasio na uwezo, wenye afya na wagonjwa, wenye  viungo vyote na wenye hawana viungo vyote, wakulima na wafugaji na kufanya watu hhapaDuniani kutokuwa sawa yaani upande wa Nyerere na wa Mwenye upande wa Nyerere ni upande wa Duniani na upande wa mwenye ni upande wa Mbinguni ni tofauti na upande wa Duniani kwa sababu Mbinguni wote tupo sawa na hakuna ubaguzi inamaana wako sawa kwa sababu Mbinguni hakuna Tajiri, wala masikini, ubaguzi wa rangi, wala hakuna utengeno kutokana na utajiri au umasikini wa Mtu. Bali Mbinguni kuna makazi ya kuwahifadhi watu wote.

Hivyo Mungu ndiye anayetoa utofauti kwa mwanadamu na ndiye anayetofautisha kati ya masikini na tajiri lakini ni Mungu huyohuyo anayefanya watu haohao kuwa sawa hakuna ubaguzi wa aina yoyoten ile mtu mwenye fedha nyingi na ambaye hana wanakuwa na hadhi ileile ya usawa.

Mbinguni hakuna cheo nitaeleza katika sura zinazofuata, kama ilivyo mimi ni wakili na uwakili wangu utbaki hhapahhapa duniani; hata ilivyo kwa madaktari,enginia, wakuu mbalimbali, wakurugenzi, mbinguni ni usawa uleule kwa sababu mbinguni hakuna kusemakwamba Fulani ni Mkuu lakini kwa Mbinguni wote ni sawa na tunahaki kwa Mwenyezi Mungu.

Kama nilivyosema kilicho nichemsha kuandika kitabu hiki ni baada ya kuona kwamba haki ambazo ni za msingi hhapa Duniani kwa upande wa Mbinguni haki hizi zinagawiwa sawa kwa sawa pasopo kuangalia rangi ya mtu, cheo wala wadhifa wa mtu, aliokuwa nao hhapa duniani bali kila kituna huduma zote hutolewa sawa kwa sawa na hiyo ndio sababu ya mimi kutunga kitabu hiki ili kuwhapa faraja wagonjwa, wazee, watu wenye maisha magumu ya duniani, walikata tamaa ya maisha kwa sababu kinaeleza kwamba  tutanyanyasika tu hhapa duniani lakini Mbinguni hakuna Manyanyaso kama hayo na utaishi maisha ya usawa bila upendeleo hata katika Biblia inaeleza kuwa kuna Razalo alikuwa masikini Duniani lakini alikuwa na taji lakekubwa Mbinguni tofauti na Yule tajiri wa Duniani ambaye alikuwa hana kitu huko aliyakosa hata tone la maji.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Maoni

Machapisho Maarufu