KUMSIFU MUNGU
SURA
YA PILI
DOMINIKA
YA 32 YA MWAKA C KUMTUKUZA MUNGU
Leo
ni tarehe 09/11/2025 nimesali Misa
Takatifu Parokia ya Inyonga na Misa hiyo Takatifu imeendeshwa na Padre mpendwa sana ambaye
sitamtaja kwani sijaomba idhini yake. Masomo ya Dominica ya 32 ya maka c ndio
pia yaliosababisha nikatunga kitabu hiki. Siku ya leo ni siku ambayo ilikuwa ni siku ya
kumsifu Mungu, kwani hata masomo yote ya leo yalikuwa yamelenga sifa na utukufu
kwa Mwenyezi Mungu na ndio sababu kubwa iliyonichechemsha mpaka nikatunga
kitabu hiki kinachoitwa
MUNGU ANASIFIWA MUDA HUU NA MALAIKA NA WATAKATIFU MBINGUNI
UNGANA
NAO KUPITIA PAMBIO ZA SIFA NA UTUKUFU .
Kilichonichechemsha
mpaka nikatunga kitabu hiki ni baada pia ya kurejea kwenye kitabu changu
kngine chenye kichwa cha habari
TUMSIFU,
TUMWABUDU NA TUMSUJUDIE MUNGU
Nimeelezea
bayana namna ambavyo Mungu anasifiwa mbinguni. Na nimeeleza bayana kwamba Mungu
aliumba mwanadamu, si kwa ajili ya kwamba mwanadamu amsifu Mungu hapana maana
kabla ya Mungu kumuumba mwandamu huko mbinguni kulikuwa na viumbe wanaomsifu na
kumtukuza na kumwabudu Mungu. Viumbe hao walikuwa wanatosha kabisa kumsifu na
kumwabudu Mungu. Mungu alimuumba mwanadamu kwa kwa lengo la kuungana na viumbe hao wengine waendelee
kumsifu na kumtukuza Mwenyezi Mungu, ila sio kwamba alimuumba kwa ajili ya
kwamba mwanadamu amsifu na kumwabudu Mungu. KAMA INGEKUWA HIVYO BASI BINADAMU
WOTE WANGEENDA MBINGUNI.
Maneno
haya yanaunga mkono kitabu changu kingine nilichotunga kinachitwa,
KUMUONA
MUNGU (UTAKATIFU) NI KAZI
JINYIME
YA DUNIANI UPATE TIKETI YA KUMUONA MUNGU
Hii
inanesha kuwaoona viumbe wanaomsifu na kumwabudu Mungu Mbinguni ni kazi maana
sio wote walioteuliwa kushuhudia Mungu akisifiwa na Malaika na Watakatifu
Mbinguni ambao hutumia vifaa mbalimbali
vya kumsifu , kumtukuza Mungu , kama vile kengele, kinubi, vinanda. Na wanapiga
piga vitu mbalimbali vinavyotoa sauti nzuri inayompendeza Mwenyezi Mungu huku
wakiinua macho yao juu na wengine wakiwa wamelala kifudi fudi huku wakiwa
wanamsifu Mungu aliye waumba na Mungu
wakiwa wamemweka katikati na huku akiwa amezungukwa na viumbe vya ajabu ambavyo
vimeumbwa na Mungu mwenyewe na viumbe vingine vinachezea vinanda katika hali
inayoleta furaha isiyo na kifani mbele ya kiti furani cha ajabu ambacho
hakielezeki na kukiona tu unapata raha ya ajabu. Huku wengine wakiwa
wanamzunguka Mungu wakifurahi tu kumuoona na wengine wakiwa wanashuhudia jinsi
Mungu akiwa anasifiwa.
Wapo
watakatifu ambao hawajatangazwa na Baba Mtakatifu Yeyoye Yule nao wanashuhudua jinsi Mungu anavyosifiwa na
wao wenyewe wanamifu Mungu. Kuna kiumbe
furani cha ajabu kinachezea na kupiga kinanda kwa ustadi wa hali ya juu sana na
kitu furani kinapulizwa vyema hali ambayo inaleta furaha kubwa sana Mbinguni. Mungu
Muumba wa vitu vyote vinavyoonekana na
visivyoonekana akiwa anaona jinsi gani anavyosifiwa. Na huku malaika watakatifu
wakiwa wakishuhudia pamoja na watakatifu wengine kwa namna ambayo inaleta raha
na furaha kubwa mno. Kwa upeo wangu mwenyewe mimi mwandishi nimeshindwa namna
ya kuelezea ila kama umenielewa ni furaha isiyo na kifani na haifananishi na sherehe, tafrija, mkesha
wowote ule hata sherehe zisizo na kifani
za ulaya au bara loote lile hazifiki hata chembe ya mchanga mdogo.
Hii
ni kwa namna ambayo sitaweza kuielezea ambavyo ipo, lakini ni namna ambayo
inaleta shangwe kubwa sana kuliko shangwe yoyote ile ambayo ipo duniani au kokote
kule duniani au kwenye sayari yoyote ile.
Hii
ni shangwe na sherehe na tafrija kubwa sana ndio maana hata katika bibilia
imeeleza bayana kuwa siku moja mbinguni
ni sawa na miaka elfu moja . Soma 2 petro 3.8.
Mungu ndiye wa ajabu na mwenye utakatifu
mkubwa sana kuliko kiumbe chochote duniani kuwahi kutokea. Ndio maana kama
nilivyoeleza hapo awali kwamba kwa Mungu
miaka elfu moja ya duniani ndio sawa na
siku moja iliyoisha tu yani ya jana. Nimejifikirisha na nimemuona
Mwenyezi Mungu kwa namna ambavyo malaika hao wanamsifu Mungu akiwaona, lakini
Mungu sijamwona maana ukimuuona Mungu basi unakufa.
MUNGU ni Roho,” na wanadamu hawawezi kumwona. Hayo ni kutokana
na maandiko katika Yohana 4.24. Hata hivyo, Biblia inataja watu ambao walimwona
Mungu kwa njia Fulani. Soma Waebrania 11.27
Linganisha hali yetu na ya mtu aliyezaliwa kipofu. Je, upofu
wake unamzuia kabisa kuelewa mambo yanayomzunguka? La hasha. Mtu aliye kipofu
hupata habari kupitia njia mbalimbali zinazomwezesha kutambua watu, vitu, na
shughuli zilizo karibu naye. Mwanamume mmoja kipofu alisema hivi: “Mtu haoni tu
kwa macho. Akili inahusika pia.” Ndio maana mtu aliyezaliwa hana macho huenda
shule, na ana haki ya kuwa na familia kama wengine.
Vivyo hivyo, ingawa huwezi kumwona Mungu kwa macho halisi,
unaweza kutumia “macho ya moyo” wako kumwona. Mimi mwandishi wa kitabu hiki,
pale pia ambapo ninapomuomba Mungu anikinge na anilinde na maadui zangu hasa
hasa wa njia ya kelekea Tabora, huwa nafumba macho na kuvuta taswira kwa
ukaribu huku nikivuta imani kubwa kuwa Mungu ananioona na ananipigania na adu
hao. Ndio maana kila wakiweka mitego hainasi , kumbe mitege hiyo wanajiwekea
wenyewe kupia Mungu mwenyewe.
Hata katika kitabu changu kingine chenye
kichwa cha habari
MUMGU
YUPO KWELI, MAAJABU YA MUNGU KATIKA UUMBAJI WA DUNIA, niijaribu kuweka picha ya
Mungu niliikosa kwenye mtandao bali niliweka picha ya maajabu tu ya Mwenyezi Mungu.
Mungu
haonekani wala hajulikani yupoje. Ni fikra tu ya kufikiri namna ambavyo Mungu
yupo. Kwa hiyo kitabu hiki kitakufaa sana. Uwe mtoto mdogo sana, wewe kaka,
shangazi, Mjomba. Wewe mtu wa Mungu. Kiongozi mkuu wa dini. Mwanajumuiya wa
mwenyekiti wa jumuia mbalimbali vigango.
Kupitia
kitabu hiki utapata baraka na neema sana
ambazo zitaongezeka moja kwa moja pia mtunzi
wa kitabu hiki naye atapata baraka na
neema kutokana na wewe kusoma kitabu hiki ambacho ametunga mwenyewe na wala
hajakopea sehemu yoyote ile.
Kadri
unavyoendelea kusoma kitabu hiki pia na mtoto wako , naye atapata baraka na
neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Kitabu
hiki ambacho kipo tofauti kabisa hakijawahi kuandikwa na mtu yeyote yule hapa
duniani. Kama wewe ni mtaalamu wa Komputa jaribu kuingiza maneno haya kwenye
komputa uone kama yana fanana na mwandishi yoyote yule. Jibu ni hapana.
Maandishi haya yatadumu kuliko hata umri wa mwandishi au msomaji na mwisho wa
kiama nitakuja niletewe kitabu hiki
mbinguni. Kwahiyo tuendelee kumwabudu na kumsifu Mungu pekee.
Najuwa
wapo watu wenye kudharau hili ambao wao kutwa nzima wanashinda kwenye mitandao kuangalia
picha za utupu na picha ambazo hazimpendezi Mungu badala ya kufuatilia na
kusambaza neno la Mungu kadiri ambavyo Mungu mwenyewe ameingia rohoni mwa
mandishi wa kitabu hiki mpaka akatunga kitabu ambacho sasa wewe mtumishi wa
Mungu uliyeteuliwa unakisoma. Maana asiye mtumishi wa Mungu kazi yake itakuwa
ni kutoa kejeri, dharau, kukashifu kitabu hiki cha Mungu badala yake yupo tayari
kutoa maoni kwenye picha za wadada ambao wamevaa nusu Uchu, wadada wadangaji
ambao viuongo vya miili vinaonekana kwa macho kinyume na taratibu. Hapo kupata
Baraka itakuwa ni ndoto.
Hata
napo napenda kuelezea jambo. Kwani kuna ubaya gani mtu akiwa ni wakili kutumiwa
na Mwenyezi Mungu kufikisha neno la Mungu?
Ukitaka
kuona kuwa kitabu hiki ni cha ajabu, kama ndugu yako anaumwa kichape kitabu hiki
alafu nyuma ya kitabu hiki andika maneno haya
MUNGU
MPONYE MGONJWA WANGU KISHA ANDIKA NA
MAOMBI YAKO ALAFU CHOMA UKURASA
ULIOONDIKA MAOMBI subiri sasa mgonjwa
wako apone.
Imani
ndio kila kitu
BARIKIWA
SANA



Maoni
Chapisha Maoni
thank you very much asante sana