MALAIKA NA WATAKATIFU WANAMSIFU MUNGU MBINGUNI
SURA
YA NNE
MALAIKA
NA WATAKATIFU WANAMSIFU MUNGU MBINGUNI.
Sura
ya tatu nimeeleza bayana vifaa ambavyo vinatumika kumsifu Mungu ambavyo hakuna
haja ya kuvitaja tena. Inaeleza bayana vifaa hivyo vinatumiwa na malaika,
watakatifu wengine akiwepo pamoja na Padri Luka.
Biblia
imeeleza bayana katika mistari mingi mingi sana ambayo itachukua muda sana
kuelezea namna ambavyo watakatifu, Malaika na wenye heri wanavyo msifu Mungu
mbinguni. Watakatifu hao wamegawanyika katika makundi mbalimbali. Kuna
wanaomsifu Mungu na kumsujudia Mungu. Kuna ambao wamelala kifudifudi. Wote lengo lao ni moja la kumsifu Mungu na kumwaga sifa kemkem kwake.
Viumbe vyote vinavyoonekana na visivyoonekana vyote vinaamini kwamba
anayestahili kupewa sifa ni Mwenyezi Mungu tu. Muda huu unaposoma kitabu changu
sifa zote zinamwendea Mwenyezi Mungu na
Mwenyezi Mungu akazipokea sifa
hizo. Muda huu unaposoma kitabu Fumba
macho kwa imani kubwa ungana na malaika na watakatifu wanaomsifu Mungu muda huu
kama jina la kitabu linavyosema kuwa MUMGU ANASIFIWA NA MALAIKA NA WATAKATIFU
MBINGUNI UNGANA NAO KUPITIA PAMBIO
Kwa
imani tunaamini malaika na watakatifu baadhi wakiwa mbele wengine wakiwa juu, wengine wako pembeni
kulia na kushoto wakiwa wanamwabudu Mungu na kumsifu Mungu.
Pia
Padre Pio ambaye pia nimetunga kitabu cha kwake ambacho kimeeleza kwamba Padre
Pio utuombee pamoja na padre Walter Luekewille ambaye naye nimeeleza kwa maisha
aliyoishi duniani ameacha alama za kikiristo miyoyoni mwetu.
Ungana
na badhi ya Watakatifu waliotangazwa na
hata wale wasiotangazwa ambao wamebeba majina ya jumuia zetu, vigango vyetu na
majina ya parokia zetu.
Somo
wangu James, wapo malaika, walinzi wa aina mbalimbali wapo viumbe wasioonekana
ambao sisi binadamu hatujui wakoje. Wote wapo kwenye mstari mmoja wa kumsifu
Mungu huku wakitoa sauti nzuri sana. Sauti zenye harufu njema na maua safi ya
kumsifu Mungu na huku wakiimba wakisema, Hosana juu mbinguni.
Sifa
na utukufu kwa Mwenyezi Mungu ambaye aliumba viumbe vyote vinavyo msifu Mungu
vimetoka kwake Yeye Mwenyezi Mungu pamoja na mtunzi wa kitabu hiki ambaye
anatumia kitabu hiki kumsifu Mungu. Na yeye mtunzi wa kitabu hiki naye ametoka
kwa Mwenyezi Mungu, na kwake Mwenyezi Mungu atakuja kurejea na kumsifu milele
na milele.
Kupitia
kitabu hiki anaamini kitapokelewa baada ya wasomaji kukisoma bure kabisa kwenye
mtandao.
Kupitia
kitabu chake kingine chenye kichwa
habari ‘Mungu ndiye tajiri wa matajiri’
naomba umuombe Mungu akupe tone ya utajiri kidogo tu kama incha tu ya ukucha
wako.
Namuomba
Mungu pia aniwezeshe siku moja mimi mwandishiwa kitabu hiki nije nipate fedha
niende nikalione kaburi la Hayati padri Luka, pamoja na makaburi ya baadhi ya
Watakatifu huko Ulaya.
Hivyo
wewe msomaji wa kitabu hiki ungana pamoja na mtunzi wa kitabu hiki katika kumsifu
Mungu pamoja na malaika Mbingun. Sisi Wakatoliki ambapo muda wa kuimba ukifika
tunaimba na kumsifu Mungu, kwani hakika sifa zote zinatakiwa sifa zote zimwendee
Mwenyezi Mungu. Hatuwezi kumlipa
Mwenyezi Mungu kwa mengi anayotufanyia
zaidi zaidi ya kuungana na watakatifu wote wa mbinguni na duniani katika kumsifu
Mungu. Kupitia vifaa ambavyo nimeeleza katika sura iliyopita.


Maoni
Chapisha Maoni
thank you very much asante sana