MATAJIRI
ORODHA
YA MATAJIRI DUNIANI
Mpendwa sana msomaji
wa kitabu changu hiki ambacho kitakupa faraja, matumaini, nakuleta kwenye
orodha ya baadhi ya watu matajiri duniani ambao huwezi hata kufungua au
kulegeza kamba za viatu vyao.
Orodha ya Matajiri
Tanzania
Sura
ya pili italeta maana nzuri ya kumuelezea MUNGU kuwa ndio tajiri wa matajiri
duniani ina maana hata hawa matajiri mali zao zote wamepewa na yeye Mwenyezi MUNGU
, orodha ya matajiri ni kama ifutavyo.
1. Mohammed Dewji (Mo Dewji) – Dola
Bilioni 1.8
Bilionea huyu kijana ni Mkurugenzi Mtendaji wa
MeTL Group, kampuni inayofanya shughuli zake katika zaidi ya nchi 10 barani
Afrika. Mo amewekeza katika uzalishaji wa bidhaa kama mafuta ya kupikia,
vinywaji, sabuni, nguo na hata usafirishaji. Mbali na biashara, Mo pia ni
miongoni mwa wafanyabiashara wachache walioahidi kutoa sehemu ya utajiri wao
kusaidia jamii kupitia mpango wa Giving
Pledge.
2. Rostam Azizi – Dola Bilioni 1.04
Rostam si tu mfanyabiashara bali pia ni
mwekezaji mwenye uzoefu mkubwa katika sekta ya mawasiliano, gesi asilia, na
mali isiyohamishika. Aliwahi kuwa mbunge na amekuwa na ushawishi mkubwa katika
siasa na biashara nchini.
3. Said Salim Bakhresa – Dola Milioni
900
Ikiwa umewahi kutumia bidhaa za Azam, basi
tayari unaujua mchango wa Bakhresa Group kwenye maisha ya kila Mtanzania.
Kuanzia kwenye chakula, usafirishaji wa baharini, hadi runinga ya Azam TV,
Bakhresa ameweka alama kubwa kwenye uchumi wa Tanzania.
4. Ally Awadh – Dola Milioni 600
Awadh amejijengea jina kubwa kupitia biashara
ya mafuta na vituo vya mafuta vilivyoenea nchini kote. Ujasiriamali wake
umemfanya kuwa miongoni mwa vijana waliofanikiwa kwa kasi katika miaka ya
karibuni.
5. Shekhar Kanabar – Dola Milioni 390
Anajulikana kwa biashara ya vifaa vya magari –
hasa betri, tairi na vipuri. Ni mfano mzuri wa jinsi sekta ya vipuri vya magari
inaweza kugeuka kuwa fursa kubwa ya kifedha kwa wenye maono.
6. Fida Hussein Rashid – Dola Milioni
145
Fida amejikita zaidi kwenye biashara ya magari
na ujenzi wa majengo ya kifahari. Anaonekana kuwa mwekezaji mahiri katika sekta
ya mali isiyohamishika.
7. Yusuf Manji – Dola Milioni 20.4
Japo amekuwa kimya kwa muda, Manji aliwahi
kutikisa jiji la Dar es Salaam kupitia uwekezaji kwenye viwanda, ujenzi, na
hata michezo. Ana historia ya kuwa mmoja wa watu waliowahi kuwekeza fedha
nyingi katika klabu za soka Tanzania.
8. Ghaleb Said Mohammed – Dola Milioni
15.3
Mfanyabiashara huyu amewekeza katika huduma za
kifedha, majengo ya kibiashara, na vyombo vya habari. Anaendelea kupanua
shughuli zake ndani na nje ya nchi.
9. Yogesh Manek – Dola Milioni 9
Amejikita katika benki, bima na huduma za
afya. Manek ameonyesha kuwa sekta ya fedha ina nafasi kubwa katika kujenga
utajiri wa muda mrefu.
10. Abdulaziz Abood – Dola Milioni 8.5
Mbunge wa zamani na mfanyabiashara mashuhuri
anayehusishwa na biashara za usafirishaji, mafuta na vyombo vya habari.

Maoni
Chapisha Maoni
thank you very much asante sana