MUNGU ANASIFIWA KWA VINUBI, VINANDA, ZEZE, KENGELE VINGWENGWE NA VIFAA VINGINE
SURA
YA TATU
MUNGU ANASIFIWA KWA VINUBI, VINANDA, ZEZE, KENGELE VINGWENGWE NA VIFAA VINGINE
Katika
hali ya kumsifu Mungu, vifaa hivi vinatumika na binadamu katika hali ya kumsifu
na kumwabudu Mungu. Vifaa hivi ni kama vile gitaa, vinanda, filimbi, tarumbeta, ngoma, zeze, marimba,
vinubi, vigenge, kengele. Ni vifaa vinavyotumika na mwanadamu wa hapa duniani katika kumsifu
Mungu.Huku baadhi wakiwa wanapiga makofi ili kusifia Mungu katika Roho ya kweli.
Vifaa
hivi hivi ambavyo vimetengenezwa na binadamu hapa duniani vikitumika vizuri
sauti yake huweza kupenya moja kwa moja na kumfikia Mwenyezi Mungu kwa imani kubwa
Mungu hupokea sifa hizo na anayetoa sifa hizo Mungu humpa fungu lake na wala
hawezi kamwe kumsahau na mwisho wa maisha yake ya hapa duniani, Mungu huyo huyo
anaweza akamwita kwake ili aweze sasa kumuoona kwa macho yenyewe(Waswahili husema
amuone LAIVE) endapo pia ataacha dhambi zake na kutubu dhambi zake na kuishi
maisha ya utakatifu.
Tunafahamu
kabisa kwamba vifaa hivi vinatoa sauti nzuri yenye kutoa hamasa zenye kuleta
raha, kumfanya mtu ajisikie vizuri hivyo vifaa vinatumika mbinguni kumsifu
Mungu. Vifaa vya muziki vipo vingi sana na vyote vimetengenezwa na mwanadamu
ambavyo pia vinaweza kutumika kumsifu Mungu pekee.
Vifaa
ivi ivi pia huweza pia kumchangamsha mwanadamu wa hapa duniani pale anapokuwa
hana furaha na hivyo kumpa faraja na vinamfanya
aburudike. Vifaa hivi vikitumika kwa lengo la kumsifu Mungu, hupokea sifa zake
kwa baadhi ya binadamu wanaojua kusifu na kumwabudu Mungu .Kwa sisi Wakatoliki
huwa kabla ya kuanza kusifu huwa tuna omba toba kupia wimbo wa EE bwana utuhurumie. Baada ya wimbo wa bwana
utuhurumie kuna wimbo wa utukufu kwa MUNGU
Hapo
wakati wa azimio ya Misa Takatifu sisi wakatoliki tunaungana na wakatoliki
wengine duniani kote katika kumsifu Mungu kupitia wimbo huo wa Utukufu kwa
Mungu Mwenyezi
Katika
wimbo huo vifaa nilivyovisema hapo juu ambavyo ni vinanda, filimbi, tarumbeta, ngoma,
zeze, marimba, vinubi, vinanda, vigenge hutumika kutoa sifa kwa Mwenyezi
Mungu. Mbele ya wana kwaya watoto waliovaa sare hucheza cheza kwa step nzuri yenye madowido wakiwa
wanaimba wimbo wa utukufu kwa Mwenyezi Mungu. Wimbo huu ambao unatumika pia kumsifu
Mwenyezi Mungu kwa yote ambayo Mungu ameyaumba au kuyafanya hapa duniani. Vifaa
vingine kama ivi vinatumika kumsifu
Mungu mbinguni. Hivyo malaika na watakatifu humsifu Mungu kupitia mpigaji
maalum wa vifaa hivyo ambaye hupiga kwa
madhumuni ya kumsifu na kumtukuza Mungu kuwa pia kuna viumbe wasioonekana nao
humsifu Mungu kwa namna yake viumbe hao wakiwa kifudifudi huku viumbe hao wakimsifu Mungu kwa
kumpigia kelelza shangwe Kelele hizo za
sifa huwa zipo katika mchujo wa sauti nzuri, nyororo yenye kuvutia, zenye kutia
hamasa ambayo Mungu hupendeza kuzisikia tu. Viumbe hao wasionekana huungana pia
na Watakatifu na malaika wa mbinguni ambao
humsifu Mungu na kumtukuza kupitia vifaa hivi vya kumsifu na kumwabudu Mwenyezi
Mungu. Na hivyo kufanya zoezi zima la kumsifu Mwenyezi Mungu lilete maana nzuri
ya kumsifu na kumwabudu Mungu.
Viumbe
hao wasioonekana pia watafikisha kitabu hiki cha kumsifu Mungu ili pia Mungu
aweze kuyakubali maombi kumi ya mwandishi aliyoomba na kutia nia na hatimaye kuyachoma
juu ya Mlima Itwele.
Zoezi
hili la kumsifu Mungu kwa kuungana pamoja na Watakatifu na Malaika wa Mbinguni
hata wewe mwanadamu ambaye upo duniani unaweza ukatumia muda wako mzuri wakati
wa uhai wako kumsifu Mungu na kuungana na malaika na watakatifu kupitia zeze na
vinanda . Mungu anasikia sauti nzuri inayompendeza YEYE Hatimaye, baada ya
kumsifu Mungu sasa unaweza ukaomba lolote lile na Mungu kupitia Mungu mwenyewe
atapokea maombi yake yote, na Mungu atakusamehe dhambi zako zote na mwisho wa
siku utafika katika ufalme wake. Pia
sifa za kumsifu Mungu zitakusaidia kupata mema yote yanayostahili duniani


Maoni
Chapisha Maoni
thank you very much asante sana