MUNGU HUZIOONA DHAHABU KWA MACHO YAKE
SURA YA NNE
MUNGU ANAJUWA DHAHABU ZIPO WAPI
Ni ukweli ambao haupingiki na ukweli wowote kuwa
kwa Mwenyezi MUNGU ndiye aliyeumba madini yote yanayoonekana na yasio onekana pia
anajuwa madini haya yapo wapi. MUNGU huyatazama madini moja kwa moja tofauti na
sisi binadamu ambao tunatumia vifaa mbali mbali kuyatafuta baadhi ya Madini
ambayo pia huenda tusiweze kuyapata au kuyaoona.
Hayo ni moja ya maajubu ya Mwenyezi MUNGU.
Ni sawa na wewe msomaji wa Kitabu hiki kama una
mali umeizificha mahali lazima ujue kwamba mali hizo umezificha au umeziweka
wapi na wala huhitaji usaidizi wa namna
yoyote ile kwani mali hizo unakuwa unajuwa umezihifadhi wapi.
Huo ndio ukweli usiopingika kwamba katika dunia hii
kuna mali nyingi sana ambazo ni MUNGU pekee anajuwa mali hizo za gharama zipo
wapi. Mwandishi wa kitabu hiki ameoteshwa kwamba ndani ya Tanzania kuna mawe ya
dhahabu ambayo yameshikana yenye matani kwa matani ambayo yakibahatika kuonwa
basi Tanzania inaweza kuwa ya kwanza kwa utajiri. Ila Muda haujafika wa kuweza
kufahamu huo mwamba wenye madini yenye thamani.
Na ndio maana machimboni huwa kuna kuwa na waganga
wa kienyeji ambao huwa wana angua kuwa sehemu furani kuna madini wana mchanja dawa
huyo mtu anaenda kuchimba. Ila kwa kuwa mwandishi wa kitabu hiki haamini
waganga hao anaamini kuwa huo ni Wizi kama wizi wingine kwani kama mganga
anajuwa hayo madini yapo wapi si aende mwenyewe akachimbe.
Hivyo ninao uthubutu wa kumsifia Mungu kuwa yeye
ndiye tajiri wa matajiri wote duniani hapa na huko kwingine .
Mfano halisi tunao, hata uwe mwema kiasi gani
huwezi kumpa jirani zako mali zako zote. Mfano huo ndio mfano hai. MUNGU hawezi
kumpa binadamu utajiri wote wa hii dunia maana ni ukweli usiopingika kuwa MUNGUanaogopa
kumpa binadamu utajiri wote kwani ndio atakuwa anampoteza huyo mtu badala ya
kumpata.


Maoni
Chapisha Maoni
thank you very much asante sana