MUNGU NDIYE TAJIRI WA MATAJIRI
SURA YA TANO
MUOMBE MUNGU AKUPE SEHEMU YA UTAJIRI
Ni ukweli usiopingika kuwa vitu vyote ni vya
Mwenyezi MUNGU na kwake mbinguni tutarejea na kuviacha, ila msomaji wa kitabu
hiki Muombe MUNGU aweze kukupa hata
chembe ndogo tu ya utajiri wa mwenyezi MUNGU ili na wewe uishi kama
binadamu wengine. Ukifuatilia pia vizuri sio kila kitu unachomuomba mwenyezi MUNGU
anakupatia kwa wakati. La hasha. Kuna wakati muda wa kupatiwa unachomba unakuwa
haujafika na nakuomba usikate tamaa maana Mungu hajibu siku moja.
Kuna wakati MUNGU hampatii binadamu kile anachoomba
kwa sababu anajuwa pia akimpatia ndio itakuwa mwanzo mwisho wa huyo binadamu kumtumikia MUNGU maana ataanza
kuabudu na kutumikia mali ambazo MUNGU amempatia.
Kuna baadhi ya wasomaji watapenda sura hii ya tano
huku wakiamini kuwa ni kupitia maombi tu MUNGU atawapa utajiri. Jibu ni sio
kweli. Ninavyosema omba MUNGU akupatie sehemu ya utajiri ni pamoja na wewe
kujibidisha katika shuguri zako za kila siku kama vile ufugaji, kuuza mchele,
biashara ya genge, kuwekeza katika kilimo na kufanya shuguri mbali mbali. Sio
kushinda na bibilia ukiketi kuomba toka asubuhi hadi jioni ukisubiria miujiza
ya Mwenyezi MUNGU.
Mwandishi wa kitabu hiki anvyosema Muombe MUNGU
akupe sehemu ya utajiri anakutaka pia ufanye kazi na uwe mbunifu alafu MUNGU
sasa akutangule kwenye kazi zako za kila siku hapo utatoka kwenye hatua moja na
utaenda kwenye hatua nyingine.
Kikubwa pia n kumuomba MUNGU akupe afya njema na
afya hiyo ndio itakuwezesha wewe kupata utajiri
Basi msomajiwa kitabu changu muombe MUNGU akupe
hata kiasi kidogo cha mali au utajiriwa ahapa duniani


Maoni
Chapisha Maoni
thank you very much asante sana