MUNGU NDIYE TAJIRI WA MATAJIRI
ü SURA
YA KWANZA
ü MUNGU NI TAJIRI WA MATAJIRI
ü Kilichonishawishi mpaka kupata kichwa cha habari
hiki ambacho ni kichwa cha habari adimu duniani kote hakijawahi kutungwa hapa Tanzania
na mtu yeyote Yule, ni kwa uwezo wa Mwenyezii
MUNGU ambaye alinitokea kupitia ndoto na kupata maono kwamba natakiwa nitunge
kitabu hiki na kukiposti kwenye mitandao mara moja nisipofanya hivyo nitakufa ili
mataifa waweze kujua na kukiri kuwa MUNGU ndiye Tajiri wa Matajiri, na hii pia
ni njia mojawapo ya kumsifu, na kumtukuza MUNGU.
ü Nimetunga vitabu vitano vya kumsifu sana MUNGU,
vitabu hivyo sijakopea au kunakiri sehemu yeyote ile bali ni kipaji kutoka
kwake. Huenda MUNGU mwenyewe alitaka kufikisha ujumbe kwako wewe msomaji
kupitia Wakili James Lubus. Mimi ni
nani mbele ya MUNGU mpaka niandike vitabu mbali mbali mia moja. Maana wengi
walitamani wawe kama mwaandishi wa vitabu kama mimi wakili. Ila MUNGU ametoa
vipaji kila mtu na kipaji chake. Kuna mengine ambayo hata mimi mwandishi wa
kitabu siwezi kuyafanya ila unakuta anayayafanya mtu asiyejuwa hata kusoma.
ü Moja ya vitabu vya kumsifu MUNGU ni
ü MUNGU ANASIFIWA NA MALAIKA NA WATAKATIFU WOTE
MBINGUNI, UNGAMA NAO KUPITIA SALA NA
PAMBIO
ü MBINGUNI
RAHA, KUSIFU NA KUABUDU KILA SIKU
ü KUMUONA MUNGU(UTAKATIFU) NI KAZI
ü TUMWABUDU NA TUMSIFU NA TUMSUJUDIE MUNGU
ü KWA MUNGU WOTE NI SAWA
ü NATAMANI KUISHI BAADA YA KUFA
ü MUNGU TAJIRI WA MATAJIRI
ü NAMPENDA MUNGU NITAUNGAMA DHAMBI ZANGU NIPATE UZIMA
WA MBINGUNI
ü MAAJABU YA MUNGU KATIKA UUMBAJI WA DUNIA
ü MUNGU YUPO KWELI
ü N.K
ü Namshukuru MUNGU kwa kupata upendeleo maalumu wa
kuniwezesha mimi kutunga kitabu kipya
kinacho sema MUNGU NDIYE TAJIRI WA MATAJIRI
ü Ujumbe wa Mwenyezii MUNGU kupitia kipaji cha Wakili
JAMES LUBUS, ni baada ya kuona matajiri wengi wa dunia jinsi ambavyo
wanashindwa kumshukuru MUNGU kwa huruma yake, ambaye ameweza kuwapa Utajiri wa
kipekee mpaka wakangia kwenye Record ya Matajiri Tanzania, Africa Mashariki
na Africa hatimaye Duniani
ü Pasipokujuwa kwamba kila kinachoonekana Duniani
kimeumbwa na Mwenyezi MUNGU pekee. Sisi binadamu hata tuwe na uwezo gani huwezi
ukaunda hata ka mchicha. Kwenye kitabu changu kinachoitwa, MUNGU YUPO KWELI,
nimeeleza ukweli kwamba kila unachokiona kimeumbwa na Mwenyezii MUNGU. Ila
binadamu hawezi kutengeneza hata kiumbe chochote kile akakipa uhai.Tumesikia
Simulizi mbali mbali kuwa huko Ulaya Wazungu walitengeneza Mwanadamu anayeongea
ukimuuliza swali anajibu, hana punzi ya Mwenyezii
MUNGU.
ü Ukifuatilia masimulizi mbali mbali kuna ROBOT moja
anaitwa SOPHIA , Robort hiyo huongea na kujibu maswali lakini sio binadamu.
Hapa duniani kila kitu unachokioona kimeumbwa na Mwenyezii MUNGU na hii
inamaana kuwa MWENYEZII MUNGU NDIYE
TAJIRI WA MATAJIRI NA NDIYE muanzilishi
na muasisi wa vitu vyote unavyoviiona na visivyoonekana. Ina maana kwa
sisi Wakiristo WAKATOLIKI KUPITIA SALA ya Nasadiki kwa vitu vyote
vinavyoonekana na visivyoonekana.
ü Bado tunaamini uwa kuna viumbe vya ajabu sana
ambavyo havionekani kabisa lakini vimeumbwa na mwenyezi MUNGU.
ü Ndio maana kuna viumbe vingine kuvioona mpaka
utumie darubini kali.
ü Hivyo ukiona
tajiri anajidai na mali zake anakuwa
hajitambui tu kuwa hizo ni mali za Mwenyezi MUNGU yeye ameazimwa tu kwa Muda.
Hata mwandishi wa kitabu hiki anamiliki gari nne lakini zote hizo sio mali zake
richa ya kwamba kwenye kadi ya gari yameandikwa majina yake.
ü Pia mwandishi wa kitabu hiki anamiliki mali nyingi
tu ila hawezi kujivuna kwani vyote ni mali za mwenyezi MUNGU.
ü Tofauti sasa na mwandishi wa kitabu hiki, kuna
baadhi ya watu wanamilki mali kidogo tu ila kila siku zinawaleta majivuno na
wanajivubia kweli kweli kwamba wao wapo tofauti na wengine. MUNGU hapendi
kabisa.
ü na vitu alivyopewa na kuna vitu ambavyo wengine wamenyimwa inamaana
anajidai kwa maana vitu hivyo vimetoka kwa MUNGU kwa maana yeye ndiye anayeumba
vinavyoonekana na visivyoonekana


Maoni
Chapisha Maoni
thank you very much asante sana