SURA YA TATU
UTAJIRI KATIKA MAHITAJI MAKUU YA BINADAMU
Hivyo basi mahitaji makuu muhimu ya mwanadamu yapo
matatu ambayo ni chakula,malazi na mavazi.Ili ujitoshereze kuwa tajiri inatakiwa
umudu haya mahitaji yote na uyapate kwa upendeleo mkubwa sana . Hii ina maana
kwamba wakati baadhi ya binadamu wengine wanahangaika na kuwaza kwa undani wapi
watapata mahitaji haya matatu, wewe uliyejaliwa na MUNGU mpaka unaanza kukufuru
kwamba hee kumbe kuna watu wana shida vyingi Duniani.
Tukianza
na chakula ni ukweli usiopingika
kuwa matajiri ndio wanaongoza kula chakula chochote wanachokitaka bali maskini anakula chakula chochote kile
kinachopatikana au kinachokuwa mbele yake na haijalishi chakula hicho ni kizuri
au sio kizuri. Maskini anakula bora chakula na tajiri anakula chakula bora na
kitamu. Kuna baadhi ya matajiri wana
uwezo wa kula chakula wanachokitaka au kukihitaji hata kama chakula hicho
kinaweza kikawa kipo bara lingine yupo tayari kuingia gharama kukifuata hicho
chakula ili aweze kukipata. Hivyo yupo tayari
kwenda Ulaya kula chakula cha mchana tu kwa kuruka na ndege. Maajabu ya
mwenyezi MUNGU yapo hapa kwa matajiri. Kuna baadhi wana fedha ya kununua kila
kitu ila MUNGU naye akawanyima hamu ya
kula ambayo huwezi kuipata dukani maana
hamu ya kula huwezi kinunua duka la lolote lile la madawa. Hata wale wanaouza
vidonge vya kuongeza hamu ya kula yani Vitamai C haifanyi kazi kama hamu ya kula ya asili ya Mwenyezi MUNGU, maana
yake hamu ya kula chakula inayoitwa ‘’ apetaiti’’ hata kama ukiwa na fedha namna gani huwezi kununua apetaiti ya kula
chakula.
Upande wa malazi, malazi yanayozungumziwa hapa si
malazi ya magonjwa inamaana sehemu ya kujisitiri kama nyumba za magorofa
makubwa hata nyumba za kawaida hata ya nyasi pia ni malazi MUNGU mwenyewe ndiye
anawezesha binadamu kuwa na malazi kwa kiwango tofauti ipo kama vile vidole
ambavyo haviwezi kulingana utaifa au
rangi kama watu wenye rangi nyeupe walivyojaliwa kuwa na malazi mazuri kama marekani, uarabuni
nk, na sio Afrika kipekee nipende kumshukuru MUNGU kwa kuandika kitabu hiki
watu wapate kujua kuwa MUNGU ndiye tajiri wa matajiri duniani.
Ipo ivi maladhi ndio yanayomuonesha mtu au
yanayotambulisha utajiri wa mtu mmoja na mtu mwingine. Mtu anayetoka kwenye
nyumba ya nyasi na anayetoka kwenye nyumba ya bati lazima watu hawa wawe
tofauti kabisa.
Wengi wanatamani kweli kuwa na makazi bora ila sasa
vifaa vimepanda bei balaa na nyumba ukiipauliwa inaanza sasa kuongea kiingereza
inahitaji, tiles, skimming, bandaring, na malembo mazuri ya kisasa. Nenda
ukaulize bei ya vitu hivyo dukani ni fedha nyingi sana.
Hakuna mtu anayetaka kuishi maisha ya dhiki na
shida ni hali tu ndio haziruhusu kabisa kama nilivyosema awali kuwa binadamu si
sawa na vidole havilingani.
Na hali hiyo ndio inayomtoafutisha maskini na
tajiri japo hata maskini wenyewe nao wapo kwenye madaraja. Kuna maskini mwenye
unafauu kuliko wengine na kuna maskini ambaye hata ukimuona utasema huyu ni
Maskini. Kuna maskini ambaye hana viuongo vyote na kuna maskini ambaye ana
viungo vyote ila amekosa tu mahitaji ya kibinadamu.
Vile vile hata matajiri nao wametofautiana tajiri
kwa matajiri. Kuna matajiri ambao wapo daraja la kwanza yani hao ndio ambao
wapo kwenye orodha ya matajiri na kuna matajiri ni matajiri kwa kupata mahitaji
tu ya masingi ila hawapo kwenye orodha
ya matajiri.
Vilevile watu wenye malazi makubwa ndio
wanajulikana kama matajiri na watu wenye malazi madogo ndio wanatambulika kama
masikini wakubwa duniani. Hivyo MUNGU ndiye anayeweza kuumba vinavyoonekana na
visivyoonekana hata chini ya ardhi MUNGU anajua yaliyomo hata baadhi ya madini
chini ya ardhi mfano kwa Tanzania ukipata madini unakuwa tajiri wa dunia nzima.
MUNGU anaweza kukupa uwezo wa kumiliki madini na wapi kwa kupata madini hili liwe fundisho kwa
matajiri wote duniani pamoja na kuwepo kwa matajiri wote duniani MUNGU ndiye
tajiri namba moja duniani na mbinguni kwa
hiyo ndugu msomaji wa kitabu hiki ambacho hakikuwahi kutungwa na mtu yeyote
zaidi yangu mimi mtunzi.Natoa ujumbe kwamba utajiri wote ni wa Mungu bila MUNGU
kuamua Matajiri hao wasinge pata huo utajiri
Mfano mzuri Katavi kuna mtu alikuwa anachimba choo
akakuta dhahabu na akawa tajiri hayo ni
mapenzi na mipango ya MUNGU bila ya yeye hakuna linaloshindikana kila kitu unachokiona duniani ni mali ya MUNGU
na MUNGU kupitia uwezo aliokuwanao ndiyo
anawafanya watu kuwa matajairi.
Hakika Kila kitu unachokiona ni mali ya MUNGU
sababu kimetoka ardhini dunia bila MUNGU
ingekuwa kama jangwa nahii inapelekea
kuamini kuwa MUNGU yupo. Hata
kwenye kitabu nilichokitunga cha maajabu
ya MUNGU katika uumbaji wa dunia nimeleza kinagaubaga jinsi MUNGU alivyoweza
kuumba mbingu na dunia na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana kwa macho
moja kwa moja kwamba kimeumbwa na Mwenyezii MUNGU kitabu hicho kinapatikana.
Mahitaji makuu ya binadamu NIAOROZESHA KIFUPI UTAJIRI KATIKA MALAZI
Nilishaeleza bayana kuwa tajiri anayetambulika
katika malazi ni yule anayemiliki nyumba kali na gari kali ambavyo wengi
hawana kati ya watu yeye anamiliki gari
la kwanza duniani na nyumba zote.
UTAJIRI KATIKA MAVAZI
Tajiri anavaa mavazi ya gharama sana mavazi ya
tajiri gharama yake sawa na bajeti ya mtumishi wa serikali kwanza ameajiriwa
mpaka anakuja kustafu maana yake mawazo yake yana dhahabu jiulize hizodhahabu zimetoka wapi? Maana
yake zimetoka ardhini zimeumbwa na MUNGU.
UTAJIRI KATIAKA CHAKULA
Tajiri anaongoza kula vizuri kuliko mtu yoyote
duniani japo japo kuwa chaajabu zaidi unaweza kupewa chakula cha kutosha lakini
ikakaosa apetite ya kula na hauwezi kunununua kokote hali aliyoumba MUNGU.
Tumeongelea utajiri katika mavazi ,chakula na
mavazi chakujiuliza ni kwamba vitu vyote vimetoka wapi?Bali jibu lake vimetoka
kwa MUNGU. Hii inamaana bila nguvu za Mwenyezii MUNGU na ndio maana kitabu tulichotunga kwa MUNGU
wote tupo sawa nimeeleza bayana kwamba mbinguni hakuna masikini wala tajiri wala
hakuna wanaokula chakula kizuri au
kibaya hakuna mtu ambaye ana gari na asiye na gari mbinguni watu watu wote ni
sawa lakini kwa elimu ya duniani watu
hatuko sawa kama tajiri mtoto anaweza kusalimiwa na kupewa kiti lakini tofauti
na mtu mzima masikini mfano nimeshuhudia
mimi mwenyewe mtu mzima anasalimia mtoto
kwa sababu ya fedha alizonazo mtoto na maana kinacho salimiwa ni utajiri wake
unampa heshima lakini yote hayo huishia tu kwa tajiri wa matajiri ni Mwenyezii MUNGU
yeye ndio mwasisi yaani mwanzilishi.


Maoni
Chapisha Maoni
thank you very much asante sana