TUISHI MAISHA YA UTAKATIFU
SURA
YA PILI
KUMWONA
MUNGU NI KAZI.
Ni
ukweli usiopingika kuwa Wakristo ni wengi sana
lakini wanaoishi ukristo ni wachache sana. Na ndio maana hata kwa sisi
wakiristo wakatoliki wanaotangazwa kuwa ni wenye heri ni asilimia moja tu Hii
ni kutokana na ukweli usiopingika kuwa binadamu ni wengi sana ila wenye
ubinadamu ni wachache.
Baada
ya tafakari hiyo ndio kupitia uwezo wa Mungu ukaniongoza niandike kitabu kipya
kuonesha kwamba Kumuoona Mungu(Utakatifu) Ni kazi, jinyime ya dunia uone ufalme
wa mbinguni.
Roho
mtakatifu aliniingia ilikuwa ni tarehe
30/11/2025 ambao ndiyo mwisho wa mwezi wa kumi na moja (11). Ilivyofika
asubuhi majira ya saa kumi na mbili , Mwenyezi Mungu alinisihi niende kusali
misa zile za asubuhi sana ambazo ni misa za majitoleo maana unakuwa umejinya
usingizi mtamu ule wa saa kumi na mbili. Na ilikuwa hivi, nimeamka saa kumi na
mbili asubuhi. Katika ya usingizi mzuri na mkali sana ghafla sauti ikaja. James Amka, embu hesabu moja hadi ishirini. Nikahesabu moja
hadi ishirini nikawa nimeamka kwenda kusali misa ya asubuhi.
Siku
hiyo ya tarehe 30.11.2025 ndio chem. Chem. Ya kitabu change hiki ambacho
ukikisoma vyama na kuishi zile her inane basi automatic lazima uende mbinguni.
Pamoja
na mambo mengine siku hiyo hiyo ndio iliumba msingi wa kitabu hiki kizuri kuwa
kumbe kumuona Mungu( utakatifu) Ni kazi. Sio kwa sababu niliamka asubuhi na
kenda kanisani , hapana, kwenda kusali kanisani ni jambo jingine na utakatifu
ni jambo jingine. Mbona nimeeona watu wengi wakiamka saa kumi na mbili kwenda
kusali kanisani ila akirudi kauli zake ni kaa mtu tu ambaye hajaenda kanisani.
Maana kuna baadhi wanaenda kanisani kwa mazoea tu na wengine wanaenda kanisani
kujionesha ila kwenye kuuishi ukiristo unakuta hauishi ukiristo kama
anavyotakiwa kuishi maana ndani yake anakuwa na roho ya matusi, majibizano,
kiburi na kujikweza tofauti na mafundisho na Makatazo mbali mbali katika
bibilia.
Msomaji
wa kitabu changu , chochote kile kinachoufurahisha mwili kama vile usingizi mtamu, au roho ya uvivu inatakiwa upingane nayo.
Nenda ukasali asubuhi ili kujitoa sadaka huku ukiacha watu wengine wakifurahia
usingizi wa asubuhi. Popote ulipo kama utatumia pikipiki kama utatumia usafiri
gani, lakini kujinyima kwa ajili ya kwenda kanisani kutekeleza majukumu ya
kusalii ni heri kubwa sana na ni hazina kubwa sana
Watu
wengi wanapata baraka pasipo kujijua hizo Baraka wanapataje pataje kumbe jibu lipo
wazi ni kwa sababu wanasali kwa kujitoa . Kwa hiyo, tujitoe miili yetu kwa Bwana kwa kuamka
asubuhi kwenda kusali huku akiacha wengine wakiwa wanakoroma, wakiwa wanafurahia ile raha ya usingizi kwani
usingizi ni raha.
Mifano
hai tunayo, ipo ivi, mtu alikata tiketi yake kwa ajiri ya kusafiri alufajiri
huwa anashikwa na usingizi mzito sana. Huo ni usingizi wa saa kumi na mbili . Hali
hiyo pia ni sawa na mtu anayejitolea kuamka alfajiri kwa ajiri ya Kristo na
kwenda kusali kanisani.
Hii
inaonyesha kwamba kulala ni style nzuri sana ambayo inamfanya mwanadamu
afurahie maana kuna raha furani ambayo
mwanadamu huipata kupitia usingizi.
Sasa
unapokuwa unaenda kanisani kusali asubuhi maana yake unajitoa sadaka au ni
mafungo fulani ambayo Mungu anayapokea kama sehemu ya majitoleo yako na inakufanya wewe upate baraka fulani ambazo
wengine hawazipati. Baraka unazozipata
ni pamoja na tiketi ya kumwona Mungu.Lakini
tiketi hii ili ikamilke inatakiwa pia uwe unaziishi na zile her inane pamoja na
kutii amriza Mungu na amri za Kanisa.
Hivyo
kitabu hiki kitakufaa wewe mkiristo kwa kukusaidia kwenda kusali asubuhi na
ikane roho ya uvivu inayokutaka uendelee kulala.
Kitabu
hiki kitamsaidia hata mtunzi wa kitabu kuanza kusali asubuhi kwa ajili ya
kupata baraka na neema. Ili na mimi nisiwe kama wapiga debe stendi wanaosema
ingieni kwenye gari msafiri alafu wao hawasafiri. Katika maombi yangu,
nimemuomba Mungu anisaidie kamwe nisiwe kama wapiga debe kwenye gari wanaopiga
debe kwamba ingieni kwenye mabasi , basi likanza kudondoka wapiga bede wanabaki. Hii ina manana kuwa kitabu hiki kinisaidie
hata mimi mwenyewe kumuoona Mungu kwa kujitesa duniani na kujima.
Angalia
kava ya kitabu hiki ambacho nimechora mtu mkubwa wenye matawi mengi
Waumini Wanaofurahia usingizi wa asubuhi ni
wengi sana ila wanaoenda kusali kanisani
ni wachache sana. Katika wakiristo mia
utapata ni mkiristo mmoja tu anaye amka na kwenda kusali asubuhi. Ni ajabu sana ukiangalia wakiristo wakatolki
ni wengi sana lakini wanaojitokeza
kwenda wachache sana. Kwa hiyo tuitumie
miili yetu kuitesa kwa kuamka asubuhi ili
mwisho wa siku sadaka hii Mungu ataitumia. Kukupa wewe thawabu. Kukusaidia wewe
kukukinga na mambo mabaya pasipo wewe binafsi kujijuwa
Msomaji
wa kitabu change ninakusihi uweze kuutesa mwili wako kwa kudamka sana asubuhi
na hatimaye kwenda kusali kwa dhati kabisa huku ukiacha baadhi ya binadamu
wakiwa wamelala sisi Wakatoliki tuko wengi sana mamilioni ya mamilioni ya
Wakatoliki na duniani tupo hadi bilioni na ushee lakini
wakatoliki watakaomuoona Mungu ni wachahche sana. Nakuomba msomaji wa kitabu
hiki vumilia shida za dunia, ipo siku utamwona Mungu utafarijika.
Duniani
hakuna raha yoyote ile kwani duniani kuna mateso na dhiki za kila aina hata namna ya kuelezea shida za dunia nina
shindwa.
Yani
duniani uishi kwa shida nyingi alafu ukifa ukachomwe motoni.
Kwa
hiyo, nakuomba wewe msomaji wa kitabu changu muumini mwenzangu jitese kwa kuamka asubuhi kwenda kusali, kitanda na
mwili havinaga shukrani. Hata ulale vipi
mpaka saa sita mchana au saa saba, utaamka tu na usingizi utaisha na utapotea
utasahau kana kwamba haukulala

Maoni
Chapisha Maoni
thank you very much asante sana