TUKISEMA HATUNA DHAMBI TUNAJIDANGANYA
SURA YA PILI
TUKISEMA HATUNA
DHAMBI TUNAJIDANGANYA
Kilichonichechemsha
mpaka kuandika sura ya pili ya kitabu hiki, inayosema, “TUKISEMA HATUNA DHAMBI
TUNAJIDANGANYA”. Ni baada ya kusoma
Biblia vizuri sana kinagaubaga na kugundua kwamba kuna mistari katika Biblia
inayoeleza bayana kwamba wanadamu tumejawa na dhambi, na kwamba tukisema hatuna
dhambi tunajidanganya wenyewe, na kwamba binadamu tumezaliwa tukiwa na dhambi
ya asili isipokuwa tu, Mama Bikira Maria mkingiwa dhambi ya asili. Madhumuni ya
kuwatungia watu mbali mbali kitabu hiki ni kuendelea kuelimisha wasomaji wa kitabu
hiki kwamba sisi binadamu ni wadhambi, na hivyo ili tuweze kupata uzima wa
milele, inabidi dhambi zetu tuweze kutubu. Kwa hiyo, kitabu hiki ni meli ya
kukuvusha juu ya maji ili usizame bali ukamuone Mungu. Kwa tafsiri nyepsi
kitabu hiki kinakusaidia wewe kumuona Mungu kwa kutubu dhambi zako. Hapo
inakuwa ni kama tiketi ya moja kwa moja kutoka duniani kwenda Mbinguni.
Pia
kitabu hiki kimeeleza kinagaubaga kuwa moja ya
Sakramenti za Wakatoliki ni sakramenti ya kupata Komunio. Tunampokea
Yesu kupitia umbo la mkate na divai. Hiyo ni Imani kali ya kanisa katoliki . Yesu
Kristo anakuwa yuko ndani ya moyo wako. Na Yesu Kristo ili aweze kuwa ndani ya
moyo wako inatakiwa moyo wako wewe uwe na moyo ambao ni moyo msafi. Yesu Kristo
hapendi nyumba ambayo siyo safi, nyumba ambayo ina wageni wengi na hapo ni pale
unapo karibisha vitu vingi ndani ya moyo wako, kunakuwa na chembechembe za wizi
ndani ya moyo wako.
Chembe chembe za ushirikina, na chembe za uchawi
ndani ya moyo wako. Ndani ya moyo wako kunakuwa na kiburi na dharau ya kutokumtii,
mke au mume ndani ya moyo wako unakuwa na wapangaji wengi. Yesu anataka nyumba
iwe haina mpangaji yoyote yule. Hivyo mwandishi wa kitabu hiki anakushauri wewe
msomaji wa kitabu uondoe wapangaji wote
na baki Yesu peke yake. Njia pekee ni kufukuza wapangaji kupitia kutubu
dhambi zako na unatakiwa kuungama kwa padre.


Maoni
Chapisha Maoni
thank you very much asante sana