TUSIANGALIE PICHA ZA EX KWENYE MITANDAO

 

SURA YA TATU

KUMWONA MUNGU NI KAZI.

TUSIANGALIE PICHA ZA UTUPU KWENYE MTANDAO

Kwa Wakristo wenzangu Wakatoliki, kamwe  tusiendekeze kuangalia picha ambazo hazimpendezi Mwenyezi Mungu. Wapo baadhi ya  wakiristo wenzangu wananunua Mb na bando la kutosha  kwa ajiri ya kuangalia picha za utupu. Mungu hapendi kabisa kumuoona muumini wa kanisa katoliki akiangalia picha za utupu.

 Huwezi kabisa kupata Baraka za mwenyezi Mungu. Wapo baadhi wanadiriki kabisa hadi kukopa pesa ili anunue bandle angalie picha za utupu za wadada wanao danga ambao  wanafanya kazi za umalaya. Hiyo ni dhambi kubwa sana. Unapoangalia picha za utupu katika mitandao ya kijamii inamaana unakuwa umekengeuka kweli  kwani Mungu hawezi kukubariki kwani na wewe pia unakuwa umekuwa mshirika au muumini wa vitendo ambavyo havimpendezi Mungu.  

Hivyo huruhusiwa kabisa hata kukomonika maana Yesu hawezi kukaa nyumba moja na shetani kwani tayari kwenye nyumba yako kuna posti ambayo machapisho  hayampendezi Mwenyezi Mungu kwani ni ibada ya kumtukuza shetani.

Machapisho yanayoenda kinyume na imani za sisi Wakristo Wakatoliki kwani yana kinzana na usafi wa roho.  Post za video kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha picha za wanawake walio uchi  ni post  zinazomdhalilisha mwanamke na zinaonesha picha za uzinifu picha zinazo hamasisha uzinzi.

Hiyo ni dhambi kama zambi nyingine. Mkiristo mwenzangu! Usijiingize kwenye dhambi isiyo ya lazima kwani unakosa nini? Badala ya kupokea baraka kutoka kwa Mwenyezi sasa unapokea mikosi.

Kama una rafiki ambaye ana weka kwenye profile yake picha za uchi au za kuonesha utupu wa mwanamke basi rafiki huyo ni bora uweze ku –block.   Posti za video katika mitandao ya kijamii  zina mkufuru Mungu na kumfundisha Mungu kwamba aliumba kwa kukosea. Mungu amemtumia wakili James Lubus kukufikishia ujumbe kuwa ukitaka kumuoona Mungu lazima uepukane na tabia ya kuangalia picha za utupu mtandaoni

 Na kama una hizo link unatakiwa kuzi -block ili usije ikazioona tena. Tambua kwamba kwa sisi wakiristo  katika vitu ambavyo Mungu hapendezwi navyo ni pamoja na ibada za kumwabudu Shetani. Hii  ni  ibada za kuangalia picha za uchi mitandaoni hasa hasa wakinamama wakiwa wapo  uchi. Pamoja na picha za wadada wanao danga  danga mitandaoni.

Na wewe dada Muombe Mungu akupe mchumba wako sio unatafuta wachumba mitandaooni kwa kupost picha yako, Mungu hapendi.

Waswahili wanasema,  ‘Ndege wa kundi moja huwa  wanaruka pamoja.’ Hivyo kama wewe sio mfuasi wa Mungu basi lazima utakuwa mfuasi tu wa shetani maana  wanaofanya hayo mambo  ya kupost picha za uchi mtandaooni  ni watu wa shetani. Mkiristo mkatoriki  ninakuoomba usikubali kamwe kukosa tiketi ya kumwona Mungu kwa kuangalia vitu ambavyo havimpendezi Mwenyezi Mungu

Tafuta nyimbo za kikatoliki uweze kuzifuatilia na kuzifatisha kuziimba. Tafuta Video nzuri za kikatoliki za kusifu na kuabudu zipo mtandaoni. Hapo ndio utakuwa unatafuta tiketi ya kumuuona Mungu.  

 

Hivyo mpendwa sana msomaji wa kitabu changu, ninakuibia siri kubwa kwamba ukitaka kabisa kumuoona Mungu  nina kusihi kabisa kama una tabia ya kuweka bando kwa ajiri ya kunagalia picha za utupu na machapisho ambayo hayampendezi Mungu basi utakuwa unartafuta tiketi ya kuingia Motoni na sio ya kumuoona Mungu.

Kama una tabia hiyo unaweza ukaanza kuicha leo baada ya kusoma kitabu hiki na kama huwezi kuacha tabia hiyo basi Muombe Mungu kwa Imani kubwa atakusaidia  kwani kuendelea picha za utupu mtandaooni unakuwa unaokosa Ufalme wa Mbinguni badala yake unakuwa unatafuta tiketi  ya kwenda kwa Shetani.

Katika moja ya vitabu vyangu nilivyotunga nimeeleza kwamba Mbinguni kuna raha kubwa sana kuliko tafrija, sherehe, hafla, shangwe yoyote ile ya hapa duniani kwani

Kuna viumbe wanaomsifu na kumwabudu Mungu na ndio maana kwenye kitabu changu hiki nimeeleza kwamba Kumuoona Mungu ni kazi  maana sio wote walioteuliwa kushuhudia Mungu akisifiwa na Malaika na Watakatifu Mbinguni ambao hutumia  vifaa mbalimbali vya kumsifu , kumtukuza Mungu , kama vile kengele, kinubi, vinanda. Na wanapiga piga vitu mbalimbali vinavyotoa sauti nzuri inayompendeza Mwenyezi Mungu huku wakiinua macho yao juu na wengine wakiwa wamelala kifudi fudi huku wakiwa wanamsifu Mungu aliye waumba na  Mungu wakiwa wamemweka katikati na huku akiwa amezungukwa na viumbe vya ajabu ambavyo vimeumbwa na Mungu mwenyewe na viumbe vingine vinachezea vinanda katika hali inayoleta furaha isiyo na kifani mbele ya kiti furani cha ajabu ambacho hakielezeki na kukiona tu unapata raha ya ajabu. Huku wengine wakiwa wanamzunguka Mungu wakifurahi tu kumuoona na wengine wakiwa wanashuhudia jinsi Mungu akiwa anasifiwa.

 

 

Maoni

Machapisho Maarufu