TUSIUNGAME DHAMBI ZETU KWA AJILI YA KUKOMONIKA

 

SURA YA TANO.





TUSIUNGAME DHAMBI ZETU KWA AJILI YA KUKOMONIKA

Nimetumwa na mwenyezi Mungu nifikishe ujumbe jinsi ulivyo.

Kuna baadhi ya watu huwa wanaungama kwa ajili ya kwenda kupokea sakramenti tu baada ya kupokea sakramenti anarudia tena dhambi zake zile zile . Maana ya kuungama. Kusikitika kwa dhambi ambazo amezifanya na pia kutamka kwamba hutafanya dhambi tena. Hivyo kabla ya kuungama maana nyingine zaidi ya kufanya kwa ajili ya kwamba tu uende kukomunika. Watu wakuone na waseme na leo furani amepokea Ekaristi takatifu. Lengo la kuungama ni kwa ajili ya kujuta dhambi zako na kukiri kwamba uliyoyafanya siyo sahihi mbele ya macho ya Mwenyezi Mungu, na baada ya hapo unapokea sakramenti. Hapo hata kama ukibahatika ukafa siku hiyo hiyo baada ya kuungama na kupokea sakarament takatifu unaweza ukamuoona Mungu siku hiyo hiyo. Hivyo muombe Mungu akujalie kifo chema ambach ni kifo baada ya kuungamana kupokea Ekarist Takatifu na wewe unaweza ukamuoona Mwenyezi Mungu na sio lazima mpaka utangazwe  mwenye Heri. Kuna baadhi ya watu wametutangulia mbele ya macho ya dunia ila tunaamini ni wenye Heri. Yupo padre mmoja anaitwa Padri Luka. Matendo yake yanatuonesha kabisa ni mwenye heri na huko alipo  amuombee mwandishi wa kitabu ili Mungu apokee maombi yake kumi ambayo alisali katika mlima mwana Uholo  pamoja na barua yake aliyomwandikia Mungu ya tarehe 14.10.2025 katika mlima wa Itwelel.

Pokea sakramenti kwa mujibu wa sheria za Kikatoliki. Pale ambapo ulidhamiria kuungama kwa ajili ya kujionesha kwa watu ili upokee sakramenti na watu wote wakuone kama ulipokea sakramenti. Unafuata taratibu za Kikatoliki lakini moyoni mwako ulifanya hivyo kwa ajili ya lengo la kupokea tu baada ya kuungama na  unaendelea na matendo yako yale yale. Huu sio Ukristo.  Maana kamili ya kuungama ni kukubali kwamba umetenda kosa na hutarudia kosa. Kwa hiyo msomaji wa kitabu changu usije ukaungama  halafu unarudia makosa yale yale ni dhambi kubwa sana.  Biblia imesema kwamba tukisema hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe. Lakini tuchukulie kwamba Mungu aliweka. Mwadamu anapozaliwa na dhambi ya asili, basi ndio muda wote kufanya makosa kwa Mwenyezi Mungu.

Wapo baadhi ya waumini kila siku  dhambi ni ile ile mpaka padre anamuambia umekuja kuungama zambi ile ile. Kuna baadhi huwa wanabadirisha mapadri  na kwenda kwa mapadri wapya wengine ili wasisikie dhambi ile ile.

MUNGU AKUBARIKI SANA

 

15.12.2025

Maoni

Machapisho Maarufu