TUUNGAME DHAMBI ZETU
SURA YA TATU
TUTUBU DHAMBI ZETU.
Katika
sura hii ya tatu, nimeeleza kinagaubaga nini maana ya toba? Ni kujuta kwa kitu
ambacho mtu amekifanya ambacho kwa fikira za kibinadamu inaonekana si kitu
sahihi mbele ya macho ya Mwenyezi Mungu. Hii itakusaidia sana wewe msomaji wa
kitabu hiki ambacho nimetunga mimi mwenyewe pasipo kukopea sehemu yoyote ile
kupitia msaada wa kipaji cha Mwenyezi Mungu.
Kwa
hiyo kitabu hiki kitakusaidia wewe kutubu dhambi zako. Ina maana kitakusaidia
wewe moja kwa moja kwenda kuungama dhambi zako kwa Padre na baada ya kuungama dhambi
zako zote ulizozitenda na dhambi ambazo nyingine ambazo umeisahau. Sisi
binadamu tumekuwa ni wadhambi sana. Wakati fulani unatenda dhambi nyingine
mpaka unakuwa umeisahau na kutubu dhambi zetu na kubariki na kukusamehe dhambi
kwa niaba ya Yesu Kristo.
Nimeeleza
bayana kwamba Biblia yenyewe imeeleza bayana kwamba yatakayoweza kufunguliwa
duniani na mbinguni yatafunguliwa. Duniani na mbinguni pia yatafunguliwa
kinagaubaga tena sana kwamba Mamlaka ya Hifadhi kukusamehe dhambi. Hayakuanza
leo. Yalianza kipindi kile cha Yesu Kristo mwenyewe kabla ya kupaa mbinguni,
aliweza kumteua Kuhani Mkuu ambaye ni Petro ili aweze kuwa na mamlaka yote juu
ya Wakristo wote wa Katoliki. Na sasa hivi ndio Baba Mtakatifu ambaye kwa sasa
yuko hapa na yeye.
Sasa hivi Baba Mtakatifu amevaa viatu vya
Petro. Hivyo hivyo viatu hivyo amempatia Padri ambaye sasa anakuondolea Dhambi
.
Sasa
Mungu atakapo kuwa amekusamehe dhambi
zako zote kupitia padre na Mungu pia anaweza kukusamehe dhambi zako zote. Baba
Mtakatifu ametoa mamlaka hiyo kwa Makadinari na Maaskofu na wao wametoa mamlaka
hiyo kwa mapadri.
Ikumbukwe
kwamba Baba Mtakatifu pia naye ni padri. Askofu ni Padri, hata Kadinari pia ni
Padri. Majukumu hayo yote waliweza
kupewa kipindi kile ambacho Yesu Kristo mwenyewe kabla ya kupaa mbinguni
aliweza kutoa madaraka hayo kwa mapadri mbalimbali ambapo aliweza kuwapa
madaraka mapadri kuweza kuwaondolea watu dhambi zao.
Pindi
tu pale watu wanapokuwa wanaona wamekosea na wanatakiwa waweze kuungama dhambi
zao. Hivyo msomaji wa kitabu changu. Tukiri kinagaubaga kabisa moyoni kuwa
tumefanya dhambi. Yote uliyoyafanya hayakumpendeza Mwenyezi Mungu na hivyo
Mungu kwa huruma zake aweze kukusamehe dhambi zako zote na kukusamehe. Kupitia padri
tayari dhambi zako na kwao umeondolewa. Na hapo teyari ukimpokea Yesu Kristo.
Kupitia. Mwili. Na damu ambayo ni mkate na divai. Yesu anaingia moyoni mwako
akikuta moyo uko safi kabisa. Ni kama vile nyumba umeisha Safisha. Na sabuni na
marashi yaani usanifu ipasavyo.
Yesu
Kristo anakuja moyoni akiwa na sherehe na shangwe safi sana. Anajua yuko peke
yake na utubu dhambi zako. Kitendo cha kukusamehe dhambi zako tayari na Mungu
naye anakuwa amekusamehe. Umedhamiria kwamba na kuwa padri kuungama dhambi
kwamba yale ambayo uliyafanya sio sahihi kwenye macho ya Mwenyezi Mungu na
hivyo atakusamehe dhambi zako. Baada ya kutubu. Dhambi zako, padri atakubariki
na atakusamehe dhambi zako na pia atakupa malipizi. Maana yake ni kwamba Mungu
sasa atakusamehe na atakupa malipizi kwa kusali sala mbalimbali. Kusali Rozari.
Kutubu kusali baba yetu marangapi. Ni tofauti na sheria za nchi mfano angalia, umefanya kosa kubwa kama vile umeua
au umevunja na kuiba. Serikali itaamuru na wewe unyongwe hadi ufe au ufungwe. Kwa sheria za nchi yetu ukifanya kosa, adhabu yake ni kwenda gerezani utajutia. Lakini
Mungu alivyokuwa na huruma ukifanya kosa lako anachokifanya yeye ni kukusamehe
tu kukupa malipizi tu. Yaani hata dakika tano hazifiki.
Baada
ya kusali sala ya salamu Maria mara kadhaa
na sala mbalimbali ambazo padre atasema unatakiwa uzisali, ukipiga
hesabu ya muda hata dakika tano hazifiki.
Hata kama umeua, ukienda kwa padri
ukisema niliua padre hawezi kukukamata na kukupeleka polisi
au mahakamani. Atakusamehe dhambi zako na atakupa malipizi ya kwamba nenda
ukisali Salamu Maria mara tano na Mungu pia anakuwa amekusamehe na unapotubu. Maana yake
umekubali kwamba wewe ni mdhambi. Na Mungu aweze kukusamehe dhambi zako.


Maoni
Chapisha Maoni
thank you very much asante sana