UNGAMA KWANZA NDIO UPOKEE

 


SURA YA NNE

USIPOKEE SAKRAMENT YA KOMONIO KABLA  HUJAUNGAMA

 Mpendwa msomaji na mfuatiliaji wa kitabu changu ambacho nimetunga mimi mwenyewe. Kila sehemu kuna taratibu zake. Kwa sisi Wakiristo Wakatoliki  ambapo mimi ni mmoja wapo. Ni agizo kwamba kabla ya kuungama na kupokea sakramenti ya komoniao unatakiwa kuungama dhambi zako kwanza kwa  makosa ambayo umeyafanya baada ya kujuta dhambi zako. Sura ya tatu nimeeleza kwamba   tayari Mungu anakuwa amekusamehe dhambi zako na sasa moyo wako unakuwa safi kwa ajili ya kumruhusu mgeni aweze kuingia moyoni mwako. Mgeni huyu ni Yesu Kristo ambapo sasa anaingia moyoni mwako kwa kugonga hodi na sasa na wewe sasa kumkaribisha moyoni mwako anakuwa ni mgeni wako.
Kwa wakiristo Wakatoliki ni agizo la miaka nenda rudi karne kwa karne. Kwamba kabla ya kupokea Sakramenti takatifu inatakiwa utubu dhambi zako zote ambazo amezifanya. Angalizo endapo utapokea sakramenti kabla ya kuungama ina maana wewe unakuwa umeenda kinyume na maandiko ya Kanisa Katoliki ambayo inatokana na sheria ya Kanoni, ambayo imeeleza bayana kinagaubaga kwamba Mkristo yeyote yule amesamehewa dhambi zake mara tu baada ya kuungama. Tayari. Moyo wake unakuwa ni moyo safi na hapo anakuwa tayari kwa ajili ya kupokea Sakramenti Takatifu. Endapo umepokea sakarament kabla ya kuungama dhambi ina maana unakuwa unakula hukumu yako mwenyewe. Upo wimbo ambao huwa unaimbwa wakati watu wanaendelea kukomunika? Unasema kwamba anayekula mwili wangu bila kuungama anakula hukumu yake mwenyewe. Anayekula mwili wa Kristo kabla ya kuungama. Ina maana yeye binafsi anakuwa anafurahisha tu wale watu ambao wanamuona. Upande wa Mbinguni  anakuwa anapokea na kula ukoko wa ugali anakuwa sio Yesu Kristo. Mwili kamili wa Yesu Kristo unageuka kuwa hukumu yake yeye mwenyewe binafsi anapoenda kuupokea mwili wake.
Taratibu za kidini ambazo zimewekwa na Kanisa Katoliki zimeelezwa kwamba mtu asiye mpokeA Yesu anakosa mambo mengi sana ikiwa pamoja na vibaraka vilivyotokana na Sakramenti Takatifu ya Komunio. Kwa hiyo anayeweza kupokea Ekaristi Takatifu bila kuungama anakuwa anafanya kosa mbele ya Mwenyezi Mungu kwani anakuwa anawafurahisha tu watu  ili watu waweze kumwona kama ni mkristo mzuri ambaye anatekeleza taratibu za kupokea sakramenti kama zilivyo kwenye dini . Hata wenzetu waislamu wana nguzo  za Kiislamu
Hata sisi wakiristo wakatoliki tuna nguzo  ambazo ni Skrament mbali mbali na moja ya Sakrament hizo ni kitubio na Komunio ya kwanza. Ni Sakramenti Takatifu ambazo mtu anazipata baada ya kuungama dhambi zake zote na kusamehewa na Mwenyezi Mungu. Mungu sasa moyo wake unakuwa ni Moyo Mtakatifu tayari kwa ajili ya kumpokea mgeni kama nilivyoeleza katika Chapter ambazo zimepita msomaji wa kitabu changu. Cha kuomba kwamba. Najua ungama dhambi usipokee. Kuna baadhi ya wakiristo wenzangu  wanajidanganya bure.
 Wanasema kwamba hamna haja ya kuungama kwa padre bali unatakiwa kusali sala ya majuto ambayo ni
’Mungu wangu najuta dhambi zangu zote, kwasababu nimekukosea na kukukasirisha wewe, muumba wangu Mwenyezi, Baba yangu na mkombozi mwema, usinitupe wala usinikatae, nataka kuacha dhambi na nafasi zangu zote zinazonifanya nitende dhambi, ili nishike maagano haya, AMINA.”
 
Au sala ya Nakuungamia
Nakuungamia Mungu Mwenyezi; nanyi ndugu zangu, kwani nimekosa mno kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo na kwa kutotimiza wajibu. Nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana. Ndio maana nakuomba Maria mwenye heri, Bikira daima, Malaika na watakatifu wote, nanyi ndugu zangu, niombeeni kwa Bwana Mungu wetu.
Mungu Mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu, atufikishe kwenye uzima wa milele. Amina
 
Sio  njia mbadala ya sacrament ya kitubio. Sala hizo unaweza ukazitumia kama huduma ya Mungamo haipo au padre hayupo jirani na una hatari ya kufa bila kutubu.
Tujiulize kama kulikuwa na sala hizo kulikikuwa na maana gani ya sacrament ya kitubio? Sala ya majuto, nakuungamia na sala ya Bwana utuhumie  sio mbadala wa  sacrament ya kutubu.
 Hizo ni sala za kawaida ambazo wakati uko mbali na padri, unaweza kusali sala na Mungu kwa huruma yake akusamehe. Siku hizi baadhi ya Mapadri wamekaa tu bila kuwa na kazi ya kuwaungamisha watu maana padre hawezi kukufuata nyumbani kwako akuite uende ukaungame dhambi zako. Yani dhambi utetnde mwenyewe alafu padre akufuate nyumbani kwwako. Labda uwe unaumwa tu.
Kwa kuhitimisha, topiki hii nimetumwa kutoa ujumbe kwamba  tusipokee sakramenti kabla ya kuungama. Mjumbe hauuwawi. Isije mwisho wa siku ukasema Wakili hakukufikishia ujumbe.

Maoni

Machapisho Maarufu