UTAKATIFU (KUMUNA) MUNGU NI KAZI
SURA
YA TANO
UTAKATIFU
NI PAMOJA NA KUACHA DHAMBI YA KUSEMA UONGO
Msomaji
wa kitabu changu hiki ambacho kama ukifuata haya ninayokueleza, hakika utapata
tiketi ya kumwona Mungu
Katika dhambi ambazo zinawatesa mno binadamu ni pamoja na dhambi ya kusema uongo
ambayo ni dhambi inayotesa wakiristo wengi kwa sababu dhambi ya uongo imekaa
katika sehemu tatu ambazo ni kiuchumi, kisiasan akiutamaduni. Kupitia uongo, mtu anaweza akajipatia kipato
ambacho sasa kinaweza kuisaidia familya yake na mapato mengi ya shuguli binafsi
za binadamu yanatokana na kusema uongo. Dili zote za mitaani zinapatikana
kupitia kuvunja amri ya Mwenyezi Mungu ambayo imesema usisieme Uongo maana watu
wengi wanajipatia riziki kupitia uongo.
Hivyo
ungo unampatia mtu chochote kitu. . Mtu Anaweza pia akimdhihaki Mungu kupitia
uongo kwa kujifanya anasali sana.
Hivyo
ili kumuoona Mungu mimi na wewe inatakiwa tujiadhali na dhambi ya Uongo. Hivyo
msomaji wa kitabu change hiki ninaomba tusiseme uongo ili tuweze kukuooona
Mungu.
Watu
wengi huwa wana idharau sana hii amri ya Mungu ya kutokushuhudia uwongo na
wanachukulia poa sana. Mungu sio mwanadamu alichokikataza lazima ukifuate
Kuna
baadhi ya wasomaji watasema mbona huyu ni mwanasheria na wanasheria kusema
uongo ndio mahali pake! Nani kakwambia. Kupitia
Roho Mtakatifu Mungu amenituma nitunge kitabu hiki ili
ujiepushe na dhambi ya uongo.
Hata
wewe msomaji wa kitabu hiki pia uweze kujiepusha na dhambi ya uongo. Mungu
aliweka amri zake ili ziweze kufuatwa na sio kupuuziwa. Utakatifu ni kazi mno na hivyo ili uweze
kuingia mbinguni inabidi uepukane kabisa na kusema uongo. Inabidi sasa uende kujifunza
kusema ukweli. Na ukweli wa dhati
unamuweka mtu huru kabisa. Kuacha uongo ni kazi. Anza kwa kuacha uongo pale
panapokutaka useme uongo sema ukweli kabisa na Mungu atakusaidia. Kuna ukweli mwingine ukisema lazima ukose
fedha. Ukisema ukweli pia lazima ukose utetezi. Kuna ukweli mwingine ukisema
lazima ufukuzwe kazi. Kuna ukweli mwingine ukisema lazima ukuletee madhara
mengi N akuna ukweli mwingine ukisema lazima ufungwe. Ila bora ufungwe na uje
utoke kuliko kuuokosa ufalme wa mbinguni.
Kuna
ukweli mwingine ukisema lazima ufungwe jela.. Hivyo taratibu kubaliana na
madhara utakayoyapata. Mungu mwenyewe ndie atakae kulipa madhara hayo
utakayokutana nayo.
Mimi
na wewe sasa tumuombe Mungu atusaidie
kuepuka dhambi ya uongo ambayo itatufanya pia tusimuoone Mungu. Kwa hiyo, msomaji wa kitabu hiki kizuri.
Utakatifu ni kazi kubwa sana. Vumilia mateso yatapita tu kwa wakati yatakuwa ni
mateso ya muda mfupi sana. Na hivyo
nakualika sasa uombe huruma ya Mwenyezi Mungu kwa kuungama dhambi kwa padre. Na Padri atakusamehe makosa
yako kwa kusema uongo ambao umefanya wewe ukapata mali nyingi. Uongo ambao
umefanya wewe ukatoka kwenye hatua moja kwenda hatua nyingine. Lakini mwombe
Mungu akupe riziki mbadala ya kusema uongo. Mungu mwenyewe alikuwa na maana
yake kusema kwamba usiseme uongo.
Kama
nilivyosema kwenye dhambi moja pia inatakiwa uzishike na kuzitii amri nyingine
za Mungu
BARIKIWA
SANA
Sasa
Mwenyezi Mungu kazi zako za vitabu vitano ulivyoniagiza nimemaliza vitabu vyako na sasa naomba unijibu maombi niliyoomba
katika Mlima Itwelele pamoja na maombi kumi niliyoomba katika mlima mwana
uholo. Asante sana. Vitabu vyenyewe ni
ü NAMPENDA
MUNGU NITAUNGAMA DHAMBI ZANGU NIPATE
UZIMA WA MILELE
ü
MUNGU ANASIFIWA NA MALAIKA NA WATAKATIFU
WOTE MBINGUNI, UNGAMA NAO KUPITIA SALA
NA PAMBIO
ü
KUMUONA MUNGU(UTAKATIFU) NI KAZI
ü
TUMWABUDU NA TUMSIFU NA TUMSUJUDIE MUNGU
ü
KWA MUNGU WOTE NI SAWA
ü
MUNGU TAJIRI WA MATAJIRI
ü
31.12.2025
LITANIA YA MTAKATIFU
PADRE PIO.*
*Bwana, utuhurumie.*
*Kristo, utuhurumie.*
*Bwana, utuhurumie.*
Kristo, utusikie.
*Kristo, kwa neema
utisikie.*
Mungu Baba wa
Mbinguni,
*utuhurumie.*
Mungu Mwana, Mkombozi
wa dunia,
*utuhurumie.*
Roho Mtakatifu Mungu,
*utuhurumie.*
Utatu Mtakatifu, Mungu
Mmoja,
*utuhurumie.*
Maria Mtakatifu,
Bikira Safi, *utuombee.*
Mtakatifu Padre Pio wa
Pietrelcina, *utuombee.*
Mpendwa wa Mungu,
*utuombee.*
Mwigaji wa Yesu
Kristo, *tuombee.*
Mchungaji mzuri wa
watu, *utuombee.*
Mfano wa makuhani, *utuombee.*
Mwanga wa Kanisa,
*utuombee.*
Mwenye kuabudu
Sakramenti Takatifu, *utuombee.*
Mwana mwaminifu wa
Mtakatifu Fransisko, *utuombee.*
Uliyetiwa alama na
unyanyapaa wa Yesu, *utuombee.*
Mgonjwa katika mateso,
*utuombee.*
Msaidizi wa wanaokufa,
*utuombee.*
Mkurugenzi wa roho,
*utuombee.*
Moyo wa dhahabu,
*utuombee.*
Mtume wa rehema,
*utuombee.*
Mtenda miujiza,
*utuombee.*
Mfariji wa walioteswa,
*utuombee.*
Mpenda Rozari Takatifu
Zaidi, *utuombee.*
Msaidizi wa roho
zilizo na mashaka na giza, *utuombee.*
Mfariji wa wagonjwa,
*utuombee.*
Mfano wa unyenyekevu,
*utuombee.*
Chanzo cha hekima,
*utuombee.*
Kioo cha maisha ya
kimungu, *utuombee.*
Mpenzi wa Yesu
aliyesulubiwa, *utuombee.*
Umejiuzulu kwa mapenzi
ya Mungu, *utuombee.*
Ulitenda mema duniani,
*utuombee.*
Ulitejazwa na roho wa
kujitolea, *utuombee.*
Msaada wetu na tumaini
katika mahitaji yetu yote, *utuombee.*
Chombo cha Roho
Mtakatifu, *utuombee.*
Unatuongoza kwa
Kristo, *utuombee.*
Baba yetu wa kiroho na
mtetezi, *Utuombee.*
Taji ya utukufu
Mbinguni, *Utuombee.*
Mwanakondoo wa Mungu
unaondo dhambi za dunia, *utuepushe, ee Bwana.*
Mwana Kondoo wa Mungu
huondoaye dhambi za dunia, *kwa neema Utusikie Ee Bwana.*
Mwana Kondoo wa Mungu
huondoaye dhambi za dunia, *Utuhurumie.*
*TUOMBE:*
*Mungu Baba yetu,
Umemsaidia Mtakatifu Padre Pio kuonyesha sura ya Kristo kupitia maisha ya
upendo na kujitolea.*
*Naomba tufuate Mwanao
kwa kutembea katika nyayo za Mtakatifu Padre Pio wa Pietrelcina na kwa kuiga
upendo wake wa kujitolea. Kwa njia ya Kristo Bwana Wetu.*

Maoni
Chapisha Maoni
thank you very much asante sana