UTAKATIFU NI PAMOJA NA KUWASAMEHE WATU WALIOKUKOSEA
SURA
YA NNE
UTAKATIFU
NI KAZI PAMOJA NA
KUWASAMEHE WALIOKUKOSEA
Hauwezi
kwenda kanisani kusali bila kusali sala hii ambayo inaonesha kwamba kabla ya
kwenda kanisani inatakiwa uwasamehe waliokukosea. Hayo sio maneno yangu na
nakupeleka moja kwa moja kwenye bibilia,
MT
6;9-13
SALA
YA BABA YETU
Baba
yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike
duniani kama mbinguni.
Utupe
leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na
sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.
Nilikuwa
nafanya mazungumzo na mwanandoa mmoja ambaye alishindwa kumsamehe mme wake
lakini huku yeye alikuwa anasali mara
kwa mara. Kumbe maombi yake yalikuwa hayapokelewi kwa sababu alishindwa
kumsamehe mme wake na pia alishindwa kujishusha mbele yam me wake. Baada ya
kumwambia aweze kusamehe ndio Mungu akamfungua na akaanza kufanikiwa.
Moja kati kitu kinachowashinda watu wengi ni
kitendo cha kusamehe na kusahau kabisa,yupo mtu anakwambia nimekusamehe ila sitaki
mazoea au ukaribu na wewe tena,ndugu yangu huo si msamaha. Msamaha wa kweli ni
ule unao toka moyoni na bado mnazidi kuwa na ukaribu na upendo pia.
Yupo mtu mwingine anasema nimesamehe ila
akiongea na yule aliyemkosea hana raha kabisa anatamani amalize haraka kila mtu
apite njia yake. Hata akatokea amemuona
yule aliyemkosea unaibuka uchungu usio wa kawaida ndani ya moyo wake,au kama
amemuona anakuja njia hii basi yupo radhi kubadili njia asikutane nae bado nao
si msamaha.
Mwingine anasema nimesamehe ila ikatokea yule
ndugu aliyemkosea kapata matatizo fulani,unashangaa anafurahi ndani ya moyo
wake ila nje anaonyesha kusikitika ndugu yule kupata matatizo nao huo tunasema
hakuwa msamaha bali ni ulisamehe kinafiki adui yako akipata shida na ikiwa
ulisamehe kwa moyo kabisa ikatokea kapata matatizo unapaswa kumuombea na ikiwa
unaweza kumuona na kumtia moyo au kumsaidia katika matatizo yake unapaswa
kufanya hivyo,Na hapo ndipo tunasema kweli ulisamehe.
Yesu
anafundisha katika Mathayo 18:21-22 kwamba tunapaswa kusamehe “Sikuambii hata mara saba, bali
hata saba mara sabini,” akionyesha kwamba msamaha si kitendo
cha mara moja tu, bali ni mtazamo endelevu wa neema
Utakatifu
pia ni kazi ni pamoja na kusamehe watu
waliokukosea. Moja ya vitu vigumu hapa duniani ni pamoja na kusamehe watu
walioutesa moyo wako. Watu hao ni maadui zako ambao waliwahi kukutenda mpka
ukaonekana sio mtu sahihi kabisa katika hii dunia.
Bibilia
kupitia maandiko yake imeleza bayana kwamba inakupasa kuwasamehe wale wote
waliokukosea. Kwa Mkristo Mkatoliki utake usitake ili kumuona Mungu ni lazima
uwasamehe watu ambao walikosea.
Watu
hao ambao walikupa wakati mgumu mpaka ukakufanya uwachukie hata ndugu zao na
wote ambao wanandamana nao. Watu hao
huenda walikutakana mbeley aumati wa watu mpaka utu wako ukadhalilika ila Yesu
Kristu anakutaka watu hao uwasamehe kabisa.
Nimeeleza
kila kitu kuwa UTAKATIFU NI KAZI, moja ya kazi hii ngumu ni kukutaka wewe
msomaji pamoja na mwandishi wa kitabu hiki kuwasamehe wale wote waliokutenda
kwa namna moja au nyingine.
Na
ndio maana njia ya kumuoona Mungu ni njia nyembamba kweli kweli maana duniani
inakuwa ni njia ngumu sana ambayo watu wengine ambao hawawezi kusamehe watu
walio wakosea hawawezi kuingia mbinguni.
Kusamehe
ni kusamehe tu na haijalishi adui huyo amekukosea kiasi gani unachotakiwa ni
wewe kusamehe waliokukosea na ukimaliza tu kusema nimekusamehe na Mungu naye
automatiki anakuwa amekusamehe dhambi zako. Hivyo kabla ya kusamehe omba Mungu
akusaidie uwe na moyo wa kusamehe.
Kuna
watu wengine huwa wanasamehe juujuu tu huko sio kusamehe bali ni kusamehe
kinafiki maana bado una duku duku moyoni mwako. Hapo unakuwa haujasamehe. Muombe
Mungu akupe moyo wa kusamehe ili uwasamehe kweli kweli hao wote ambao
wamekukosea. Mungu naye anakusamehe dhambi zako hapohapo.
Kumbuka
kuwa wakiristo wote Baba yetu ilivyo kwamba utusamehe dhambi zetu kama sisi
waliotukosea. Kupitia sala ya Baba yetu na kutaka wewe sali sala, uwasamehe
wewe watu waliokukosea na kuwasamehe. Ni jambo la kujinyima kwamba ya duniani
yatapita. Kwa hiyo. Msamaha uwe na amani ya moyo badala ya kusamehe pale moyo
wako unakuwa na amani. Ni kweli unakosea sana. Hamtendei haki. Kuna wengine
wanatumia mali zao kudhalilisha. Kwa kupitia kitabu hiki. Nitamke kwamba
nimeamua kumsamehe. Kitabu hiki ni kutoka moyoni kweli kweli na ni kweli
kupitia matusi. Siko karibu na hata wale watu ambao anafanya nao kazi kwa
ukaribu. Mungu alinipa kitu fulani. Nikaona sasa hapa nitumie nafasi hii kuweza
kusamehe na kusamehe kuona Ufalme wa Mbinguni. V. Neno kusamehe inatakiwa
litoke ndani na nje. Neno hili linatoka ndani ya moyo wangu wote duniani.
Lazima yatimizwe. Siwezi kubaki na kinyongo. Kuyachukia baadhi ya watu kwa
sababu tu mtu mmoja anaweza kunitukana. Mungu aweze kunipa moyo wa ujasiri kama
nisamehe na kusamehe kwelikweli. Na kusamehe maana yake ni kutamka kwamba
nimemsamehe.

Maoni
Chapisha Maoni
thank you very much asante sana