TUWAPENDE NA TUWASAIDIE WAZAZI WETU

 

SHUKURANI NA PONGEZI

Kwa moyo wa utiifu na unyenyekevu ninapenda kumshukuru MUNGU kwa kunipa uzima ambao umeniwezesha kutunga vitabu 68 maana bila wa uwezo MUNGU  Kitabu hiki kingekuwa ni bure kabisa.  .

Katika moja ya vitabu nilivyotunga ambacho kina kichwa cha habari “ AFYA YAKO NDIO MTAJI WAKO’, afya hiyo anayoitoa ni MUNGU pekee. Afya hiyo hiyo ndio inayotusaidia kumtumikia MUNGU na kuitumikia serikali. Bila afya sisi binadamu tutakuwa tunashinda tu kitandani.

Shukurani nyingi za kipekee zimwendee Padri Wilbroad Tangi kwa mema mengi ambayo amenifanyia ambayo siwezi kuyataja humu.  Sina cha kumpatia chochote  zaidi ya kumwombea kwa Mwenyezi MUNGU afya njema  na mafanikio mema.

KUHUSU MWANDISHI

JAMES LUBUS ni Wakili  aliyesajiriwa kwa mujibu wa sheria za Mawakili. Mwandishi wa kitabu hiki pia ni kiongozi wa Mawakili wa Kujitegemea na Mawakili wa serikalini kupitia barua ya uteuzi.

Mwandishi wa kitabu hiki amefanya kazi katika mabaraza ya ardhi kwa muda wa miaka  15 na hivyo ana uzowefu mkubwa sana katika masuala ya ardhi kwani ameshinda kesi za ardhi kwa asilimia 90.

Mwandishi wa kitabu hiki ametunga vitabu mbalimbali na husaidia kuwaandikia watu wengine  vitabu vyao kwa muda mfupi mno. Lubus pia hubadilisha matukio mbalimbali kuwa vitabu. Wakili  amesoma katika Vyuo vikuu mbalimbali na ana Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini. Mbali na hapo pia ana  STASHAHADA  ya Uzamili ya Sheria Mwandishi wa Kitabu hiki bwana Lubus ametunga na kuandaa vitabu vifuatavyo

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

YALIYOMO

BARUA YA PONGEZI KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS. 3

BARUA YA PONGEZI TOKA OFISI YA WAZIRI MKUU.. 3

CHETI CHA USAJIRI WA KAMPUNI YA USHAURI. 4

SHUKURANI NA PONGEZI 6

KUHUSU MWANDISHI 6

SURA YA KWANZA.. 9

WAHESHIMU WAZAZI WAKO ILI UCHELEWE KUFA. 10

USITAFUTE MCHAWI WALA MGANGA.. 11

SURA YA PILI. 15

MPIGIE SIMU MZAZI WAKO.. 15

SURA YA TATU.. 16

MZAZI NDIO MGANGA.. 16

SURA YA NNE.. 21

BIASHARA HAZIENDI KAMA HUMUHESHIMU MZAZI. 21

 

 

 

 

 

 

 

SALA YA KUWAOMBEA WAZAZI WAKO AU WALEZI WAKO.

BILA WAO USINGEKUWEPO.

Mungu wetu uliyetoa amri tuwapende, tuwaheshimu,tuwatii na kuwasaidia Wazazi na Walezi wetu, usikilize Sala tunazokutolea, kwa kuombea Wazazi na Walezi wetu, wanatufanyia mema mengi hata hatuwezi kabisa kuwalipa sawa. Tangu Utoto wetu wanatulinda, wanatutunza wanatupatia Chakula na Mavazi, wanatuangalia Mchana na Usiku. Wanachoka wanakosa usingizi wapate kutulinda na kututuliza, wanahangaika sana na hata kupata uchungu kwa ajili yetu.

Ee Mungu, uwarudishie mema yote wanayotufanyia uwabariki na kuwalinda Roho na Mwili. Uwasaidie katika kazi zao zipate kuwafaa sana. Uwatulize uchungu wa roho wapate kufurahiwa siku zote. Uwakinge na hatari zote za Roho na za Mwili. Uwalinde waone uzee mzima na mwema, wakafurahiwe na kuona mwenendo mwema wa Watoto wao. Utusaidie nasi tuwapende sana, tuwatii siku zote, tuwafurahishe mioyo yao kwa kuwatunza na kuwaheshimu. Uwalinde siku zote za Uzee wao, wakidumu katika urafiki nawe, hatimae ukatupokee wote, pamoja Mbinguni, tupate kupendana na kufurahi katika Utukufu wako Milele.

 

 

 

 

 

 

 

SURA YA KWANZA

WAHESHIMU WAZAZI WAKO ILI UCHELEWE KUFA.

Binti mmoja alimuaga mama yake kwenda kula bata na shosti zake. Mama akasema "Haya mwanangu Mungu awe nanyi katika safari yenu" Binti akajibu "mmhh! Mama gari limejaa labda huyo Mungu akae kwenye buti kama ataweza". Binti akawasha gari nakuondoka zake. Njiani wakapata ajali wakafa wote palepale, Polisi walipofungua buti walikuta mayai trei mbili yote yapo sawa kabisa kwasababu yalikuwa na Mungu.

Binti alimdharau mzazi wake akawahi kufa. Kesi ya vijana kufa siku hizi ukilinganisha na wazee wetu inatisha sana. Imekuwa kawaida wazazi kuzika watoto badala ya watoto kuzika wazazi. Hakuna kitu kinauma kama mzazi kuzika mtoto na utovu wa Nidhamu ndio chanzo. Hii ni kwa mujibu wa Biblia yenyewe ila Kisayansi sijui. Ni utovu wa nidhamu kumtelekeza mzazi wako badala ya kumtunza.

Kumbuka amelaaniwa yule asiye watunza wakwake, hiyo ni mbaya zaidi ya wasio amini. Kumbuka walikutunza kabla hata haujaota meno nawewe watunze kipindi wanaishiwa meno usiwe kama wale wajinga kumi na mbili mpaka sasa wameshindwa kabisa kuwatunza wazazi wao wawili tu wakati wazazi wao waliweza kuwatunza wote kumi na mbili.

Ni laana kubwa sana kwa mzazi aliyebarikiwa watoto kukosa hadi hela ya Panado na wakati nyie hamkuwahi kulala njaa. Tujifunze kwa Yesu muda mfupi kabla ya kufa. Alifanya mpango wa matunzo ya mama yake. Wewe mama yako tangu upate kazi hata hajui unaishi wapi. Soma Yohana 19:26 utaona ninacho kisema. Wazazi wako wanaonekana kama waganga wa kienyeji na wakati una makabati matano ya nguo, pair mia za viatu, suti za kila rangi na mikoba kwa idadi ya nguo na rangi za viatu.

USITAFUTE MCHAWI WALA MGANGA

Ni utovu wa nidhamu kugawa zawadi kwa marafiki zako, mabosi zako, michepuko yako, girlfriend wako, boyfriend wako, wachungaji wako, Padri wako na mwalimu wako na kuwasahau walio jinyima kukupa maisha yanayo kupa jeuri ya kuwazawadia wengine. Kufanya hivyo ni kujitafutia kufa kabla ya muda timilifu.

Kumbuka kufa siyo mpaka uzikwe hata mambo yako kwenda hovyo hicho nacho ni kifo. Kuvamiwa usiku na kuibiwa kila kitu hicho ndicho kifo chenyewe ndugu. Ni utovu wa nidhamu kumdanganya mzazi wako maana imeandikwa "Waongo wote watatupwa katika lile ziwa liwa la moto na kiberiti". Ukiona kila mtu anakudhurumu, kila kazi unayopata unatimuliwa, unapata mshahara lakini hauoni maendeleo, Biashara zako haziendi, kila mtu anakupiga mzinga, magonjwa kwenu hayaishi, ujue umekwisha tupwa kwenye ziwa la moto kitambo. Ili usalimike tubu yote uliyowadanganya wazazi wako kuanzia ule uongo wa kuvunja minyoo shuleni hadi siku alivyokuomba hela ya Panado ukasema hauna. Nakushauri tu utubu hata kama wazazi wako walishatangulia mbele za haki.

Ni utovu wa nidhamu kumponda mzazi wako ili kuwafurahisha wasio jua uchungu wako. Usimponde mzazi wako kwa kumfurahisha mkeo au mumeo maana madhara yake ni makubwa mnoo. Mkeo/Mumeo hajui thamani yako kama wazazi wako wala usimuite Baba yako kimeo itakula kwako wala usimuone mama yako msumbufu utakufa mapema.

Leo hii kuna wazazi wanajuta kuzaa. Mzee mmoja anasema amekuwa maskini kwasababu alitumia gharama kubwa kuwasomesha watoto wakapata kazi na kuingia mitini na ni mwaka wa saba sasa hawajawahi kukunyaga kwao, mzazi kabaki solemba amechoka utanizani fundi saa. Ni utovu wa nidhamu kuingilia mambo ya mzazi wako hadi akakwazika. Mzee mmoja alifanya sherehe aliposikia mwanae kahukumiwa kwenda jela miaka sita, huyo bwana alikuwa msumbufu sana kwa mke wa baba yake. Mama yake alipofariki Baba alijitwalia mke mwingine, kijana akashindwa kumheshimu kwakuwa walilingana umri.

Wahenga walipo sema "Mke wa baba ni mama" walitaka kuepusha laana kwa watoto wa baba maana imeandikwa katika Kumbukumbu la Torati 27:16 kwamba "Amelaaniwa yule ambaye humtendea baba yake au mama yake kwa dharau". Kijana alikuwa anaongea hovyo juu ya mke wa baba yake akaishia jela.

Ni kheri kujikwaa kidole kuliko kujikwaa ulimi. Ni utovu wa nidhamu kutomsikiliza mzazi wako kwani wahenga walisema "ASIYE SIKIA LA MKUU HUVUNJIKA GUU" Wazazi wako wanajukumu la kukuongoza ndio maana ukaambiwa shika sana amri ya baba yako na sheria ya mama yako, soma Mithali 6:20. Kabla haujaenda kuoa bila taarifa mke akakuuwa, nakwambia soma hiyo kabla haujajichagulia mume akakutoa roho. Mithali 23:22 inasema msikilize baba yako aliyekuzaa wala usimdharau hata akiwa Mzee Hittla hakusikia maagizo ya baba yake baba akafa hawajapatana kilicho kuja kumpata Hittla dunia nzima ilijua.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Maoni

Machapisho Maarufu